Posts

RAIS JAKAYA KIKWETE AMENISAIDIA KUWAPASHA VIONGOZI WA RT NA TOC;TAIFA ZIMA LINAWAOGOPA

Image
DC asiyejali sheria za nchi 'Niliiposti habari hii 12/08/2013, JK akawapasha 19/01/2014'.  Hata hivyo Rais JK bado kuna siri hajaambiwa ya kwamba viongozi wa RT walivunja sheria NO. 12 za BMT zilizotungwa na Bunge 1967. Mtaka anadai kuwa "waziri Fenella ni shemeji yake na atamlinda, Nyambui pia ni ndugu yake wa ukoo" : Wakati nchi za ulimwengu zikiwakilishwa na wanariadha wake mahiri katika mashindano ya dunia ya riadha mjini Moscow Urusi, Tanzania imevunja rekodi ya aina yake kwa viongozi wa Chama Cha Riadha Tanzania kutangulia Moscow huku wakiwaacha wanariadha nyuma. Rais wa RT (aliyechaguliwa kinyume na katiba) bila wasiwasi, aibu wala uzalendo amekwenda Moscow wiki iliyopita huku walengwa wenyewe wa mashindano ya (World Athletic Championships) ambao ni wanariadha wanaotegemewa kupeperusha bendera ya Tanzania na kupigania medali wakibaki nyuma. Cha ajabu zaidi ni pale ambapo kiongozi huyo wa RT alipofuatana na kiongozi wa zamani wa chama hic

MAZISHI: Charles Kyando maarufu kwa jina la Tola kuzikwa siku ya Jumamosi tarehe 25/01/2014

Image
Mazishi ya aliyekuwa kocha wa mchezo wa tenisi Charles Kyando maarufu kwa jina la Tola yatafanyika kesho nyumbani kwake Mwananyamala kwa Ali Maua. Marehemu alifariki usiku wa kuamkia jana baada ya kuugua kwa muda mfupi. Mazishi hayo yatafanyika kesho kwa mujibu wa habari kutoka kwa familia ya marehemu. “Huu ni msiba kwa chama cha Tennis Tanzania na taifa kwa ujumla; pengo lake kamwe halitazibika” alisema kocha wa tenis mwenzake ndg Hassan Kassim. ‘Mwnyezi mungu ailaze roho ya marehemu mahali pema peponi amina’ Pole nyingi kwa familia, ndugu na marafiki bila kusahau Tanzania Tennis Association .

UTAIFA KWANZA: Mbio za kumbu kumbu ya hayati Edward Moringe Sokoine zitafanyika Monduli mwezi Aprili 12, 2014

Image
Mwaka huu Tanzania inaadhimisha miaka 30 tangu kifo cha aliyekuwa waziri mkuu Hayati Edward Moringe Sokoine .  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dr. Jakaya Kikwete atakuwa mgeni rasmi katika dhifa hiyo itakayofanyika kitaifa Monduli mahali alipozaliwa kiongozi huyo shupavu. Madhumuni ya kuandaa mbio hizo ni kuthamini bidii,   uzalendo na ujasiri aliotuonyesha wakati wa uhai wake. Watanzania wote wanaojali utu, haki, amani na Utaifa Kwanza mnakaribishwa katika kumbu kumbu hiyo. ‘Tujikumbushe baadhi ya nukuu zake akiwa waziri mkuu’   “Ole wake kiongozi mzembe na asiye na nidhamu nitakayemkuta: Kiongozi wa siasa hana usalama wa aina yoyote. Usalama wake ni kudra ya Mungu na Wananchi peke yake. Viongozi wazembe na wabadhirifu wahesabu siku zao. Labda tusiwajue. Hawa hatuna sababu ya kuwapa imani, kuwa tutawalinda kama vitendo vyao viovu” - Edward Moringe Sokoine, 26 Machi 1983. “Katika nchi inayojali haki na usawa, majeshi hayana budi yawe ni chomb

Msiba chama cha Tennis: TTA yapata msiba mzito baada ya kocha wake mkongwe CHARLES KYANDO (TOLA) kufariki ghafla

Image
Charles Kyando (Tola) Enzi za uhai wake Sekta ya michezo Tanzania imepata msiba mkubwa usiku wa kuamkia leo kwa kufiwa na Charles Kyando maarufu kwa jina la Tola , Kyando alifariki ghafla baada ya kuugua kwa muda mfupi. Charles Kyando (Tola) alizaliwa 1968 jijini Dar Es Salaam na wakati wa uhai wake aliwahi kucheza mashindano mbalimbali ya mchezo wa tenisi na kufikia viwango vya kitaifa kati ya miaka ya 1980 hadi 1990. Baada ya kustaafu kama mchezaji bwana Kyando alikuwa kocha wa mchezo wa tenisi na pia alikuwa mtaalam maarufu wa kusuka rakets za mchezo huo. Marehemu ameacha mjane na watoto wawili, pia marehemu ameacha pengo kubwa na isiyozibika katika mchezo wa tenisi na katika chama cha tenisi Tanzania ( Tanzania Tennis Association ). Kuhusu taratibu za mazishi na taarifa zozote kuhusiana na msiba huu tafadhali endelea kusoma blogu hii ya Utaifa Kwanza .