Posts

Yaliyojiri Sokoine Mini Marathon 2014

Image
MWISHONI mwa wiki, Aprili 12 mwaka huu, macho na masikio ya Watanzania wengi yalielekea katika Kijiji cha Monduli Juu, kilichopo Wilaya ya Monduli, mkoani Arusha, kufuatilia kumbukumbu za miaka 30 tangu kufariki kwa Waziri Mkuu wa zamani wa Tanzania, Edward Moringe Sokoine. Maadhimisho hayo yaliyohudhuriwa na viongozi wa ngazi za juu wakiongozwa na Rais Jakaya Kikwete, yaliadhimishwa kwa matukio mengi ya kukumbukwa, lakini moja ya matukio yaliyotokea katika kumbukumbu hizo, ni msimu wa pili wa mbio za Sokoine Mini Marathon mwaka 2014. Mbio hizo zilianza majira ya saa mbili asubuhi, ambapo pamoja na kuwepo kwa ushindani mkubwa, kulikuwa na matukio mengi yasiyo ya kawaida, likiwemo la wanariadha kulazimika kupisha magari. WANARIADHA WANASA KWENYE TOPE Zikiwa zimesalia takribani kilomita mbili mbio za kilomita 10 zimalizike, wanariadha walijikuta wakibadilishana baada ya njia kujaa matope huku kukiwa na mgari mengi yaliyokwama barabarani. Tukio hilo lili

MABADILIKO: Sokoine Marathon itakuwa kilomita 10 badala ya kilomita 21

Image
Tunaomba radhi kwa kufanya mabadiliko ya ghafla! Hiyo ni kutokana na mashauriano kati yetu sisi waandaaji, Chama Cha Riadha Mkoa   na wanariadha wenyewe. SABABU KUU: Imeamuliwa kwamba siyo vizuri kuwakimbiza wanariadha mbio ndefu mara mbili kwa wiki moja sababu pia kutakuwa na Ngorongoro Half Marathon April 19, 2014. Familia imeridhia ombi letu na pia imekuwa wazo zuri kwa wanariadha wazoefu ambao wanafahamu athari za kukimbia mbio ndefu mfululizo. Pia wananchi wengi sasa wataweza kushiriki Kilomita 10. Taratibu zingine hadi sasa zipo kama ilivyopangwa, ila namba zinasajiliwa katika uwanja wa Sheikh Amri Abeid Karume. Tsh: 2,000 tu kwa kusajili namba yako. ZAWADI ZITATOLEWA KWA WASHINDI.

Kenenisa Bekele: The Ethiopian superstar outruns the field in Paris Marathon

Image
Kenenisa Bekele, an Ethiopian long-distance runner and three-time Olympic champion, won the Paris Marathon on Sunday, finishing the 42.195km (26.22 miles) race in a record 2hr 5min 02secs. The previous record for the Paris Marathon was held by Kenya's Stanley Wiwott, who clocked 2hr 05:10 in 2012. The race was Bekele’s first marathon. "I didn't have much experience," Bekele said. "It was very tough but it was the time I expected.” Bekele made his move with about 25km to run and opened up a lead that may have been even more significant had he not struggled with a hamstring problem. "The hamstring wasn't good after 25km. It was cramping but it's ok. I'll feel it more in the morning," explained Bekele. He missed out on the world record, which is held by Kenyan Wilson Kipsang who set a mark of 2hr 3min 23secs in 2013 at Berlin. (FRANCE 24 with AFP)

SOKOINE MINI MARATHON 2014: Usajili wa namba za washiriki umeanza rasmi

Image
Namba zimeanza kutolewa kwa washiriki wa mbio za Sokoine Mini Marathon Km 21 na Km 2 ambazo zitatimua vumbi Aprili 12, 2014 Monduli mkoani Arusha, rais Jakaya Kikwete ndiye atakayepuliza kipenga cha kuanza mbio hizo. Ada ya namba ni Tsh: 2,000 tu, namba zinapatikana Arusha pale Uwanja wa kumbukumbu ya SHEIKH AMRI ABED KARUME na Monduli pia. Kwa washiriki wote nje ya mkoa wa Arusha wasiliana na VICTOR MACHOTA kwa 0787415864 ambaye atapokea usajili kwa njia ya simu na namba yako utajulishwa kwa SMS na itahifadhiwa hadi utakapoichukua. Mwisho wa kuchukua namba yako ni Ijumaa April 11, 2014 Arusha mjini. Kwa wale watakaosajili kwa njia ya simu tunaomba mtume hela kwa AIRTEL MANEY kwa namba ya Victor Machota, unaombwa uongezee gharama kidogo ya kutoa pesa mtandaoni. Kwa wale watakaosajili namba papo kwa papo wawasiliane na PHAUSTIN BAHA 0753860668 kwa maelezo zaidi na kwa wale wa Monduli wawasiliane na ROBERT MOLEL kwa 0753739128. Kwa ratiba kamili hapo baadae pitia

‘Jakaya Kikwete Sports Village’ kujengwa Dom

Image
Mfano wa ramani ya Center inayotarajiwa ya Dr. Jakaya Kikwete National Sports Village MAANDALIZI ya ujenzi wa kijiji cha michezo kitakachojulikana kama Jakaya Kikwete Sports Village yanaendelea vizuri, ambako tayari Ikulu, Baraza la Michezo la Taifa (BMT) na Wizara ya Michezo wametoa baraka kijengwe mjini Dodoma. Akizungumza na   Tanzania Daima , Mratibu wa ujenzi wa kituo hicho, Wilhelm Gidabuday, alisema ujenzi wa kituo hicho kikubwa na cha kwanza nchini, tayari maandalizi yake yameshafikia pazuri na Ikulu ya Tanzania kupitia ofisi ya Katibu wa Rais, imeshawapa baraka ya kutumia jina la Rais katika kituo hicho. Gidabuday alisema, wiki iliyopita walikutana na Katibu wa Rais, ambako waliwasilisha maombi yao na kukubaliwa na kwamba, kuanzia sasa kituo hicho ambacho ujenzi wake utasaidia kuinua vipaji vya michezo yote hapa nchini, kitafahamika kama kituo cha michezo cha Jakaya Kikwete (Jakaya Kikwete Sports Village). “Nidokeze tu kuwa, mipango yote inakwenda sawa, tumeshafikis

OFA: Makampuni yanakaribishwa Sokoine Marathon "Corporate Team Challenge"

Image
Kama njia ya ushirikiano na makampuni ambayo huwa inakuwa mstari wa mbele kudhamini michezo; Tunayo furaha kukaribisha kampuni zenye kutaka kushiriki na kutangaza bidhaa zao. Kwa watakaokidhi masharti wataruhusiwa kuweka HEMA la mauzo na matangazo ya bidhaa zao. Michezo ni kila kitu ikiwemo elimu, afya, ajira, biashara, utalii, diplomasia UZALENDO etc. Karibuni sana watanzania wote.

Sokoine Marathon attracts top local athletes

Image
Minister for Information, Youth, Culture and Sports, Dr Fenella Mukangara By Joseph Mchekadona 29th March 2014 Five top local athletes have confirmed their particitipation at the forth coming Sokoine Marathon slated for April 12 at Monduli in Arusha. The event’s organizer, Wilhelm Gidabuday, said yesterday that Mary Naali who competed at the India Commonwealth Games in 2010 was among them. Others are local international regulars athletes are Andrew Sambu Getuli Bayo, Dickson Marwa and Alphonse Felix. Gidabuday said there will be also several sports and entertainment activities such as traditional games and dances. There will be also sports such as javelin, mini marathon for juniors and seniors. This is the second time this event to commemorated the death of former Tanzania Prime Minister Edward Sokoine who died in a car crash on April 12,1984 at Dumila in Morogoro. Gidabuday said that last year the Minister for Information, Youth, Culture and Sports,