Posts

TOC yaigomea RT: Viwango na Vigezo kuzingatiwa

Image
Mwanariadha mkongwe Tanzania Andrea Sambu Sipe (Pichani) na Musanduki Mohamed ndio pekee waliofikia viwango vinavyohitajika, kwa maelezo ya TOC hawawezi kuachwa maana viwango wanavyo. Kamati ya Olimpiki Tanzania (TOC) imelikataa ombi la Shirikisho la Riadha Tanzania (RT) la kutumia mashindano ya taifa ya riadha kuteua timu itakayoshiriki kwenye michezo ya Jumuiya ya Madola. Mapema jana, Katibu Msaidizi wa RT, Ombeni Zavala aliiomba TOC kuvuta subira hadi watakapomaliza mashindano ya taifa yatakayoanza Julai 12 na 13 ili kujua hatima ya kikosi chao cha Madola. “RT tunategemea kutumia mashindano ya taifa ili kupata timu itakayokwenda katika michuano ya Jumuiya ya Madola, hivyo tunaomba TOC itupe muda yatakapokwisha mashindano tutapeleka kwao kikosi kamili,” alisema Zavala. Katibu Mkuu wa TOC, Filbert Bayi, alikataa ombi hilo na kusema kama RT inahitaji kuteua timu kwenye mashindano ya taifa waitumie kwenye mashindano mengine ya kimataifa na si Madola. “Hatuwezi kuw

World Cup: Mkusanyiko mkubwa wa pili duniani baada ya Olympic Games

Image
Mashindano ya kombe la dunia ni mkusanyiko nambari mbili katika mikusanyiko yote ulimwenguni, pia ni mashindano yanayoangaliwa na mabilioni ya watazamaji duniani (TV Viewers). Juni 12 mashindano hayo maarufu yataanza katika miji tofauti nchini Brazil ikimwemo Sao Paulo, Rio De Janeiro, Brasilia nk.  Ni bahati kubwa kwa nchi hiyo kubwa iliyopo Latin America kwamba 2016 pia mashindano namba moja duniani (Olympic Games) yatafanyika Brazil katika mji wenye bandari kubwa ya Rio De Janeiro.

RT safari hii mkiidhulumu taifa tutafanya mapinduzi wazi wazi

Image
Andrea Sambu Sipe Habari za kutatanisha zinasukwa za kukata jina la Andrea Sambu Sipe asiende kuiwakilishaTanzania katika mashindano ya Jumuia ya Madol a . Sambu mwezi December mwaka jana aliweza kushiriki mashindano ya DANZHOU INTERNATIONAL MARATHON nchini China ambapo alikimbia muda wa masaa 2:14:30 , muda ambao umefikia kiwango na vigezo vya kushiriki mashindano ya Commonwealth Games. Mbali na Sambu pia kuna Musa Nduki Mohamed ambaye pia amefikia muda unaotakiwa, hivyo kwa maelezo mafupi na yanayoeleweka ni kwamba ‘Hakuna mwingine zaidi ya hao wawiwili wamefikia vigezo vya kimataifa vinavyohitajika ili kushiriki mashindano hayo ambayo yatafanyika mwezi July. MASWALI MUHIMU: Kama kweli RT inataka Tanzania ipate medali lakini ikanuia kumwacha Sambu je watakuwa na maana gani? Haki ya mungu Ikulu tutagonga hodi iwapo Sambu ataachwa! Sambu ni mwanariadha pekee Tanzania aliyewahi kushinda mashindano ya dunia ya mbio za nyika; Hakuna mwingine. Angalia profile yak

Standing ovation: Sydney Gidabuday received a Varsity certificate

Image
Sydney received the Distance Runner Athlete of the Year award; Sydney had a “ Standing Ovation” for a great track season! Sydney Gidabuday and Bryan received their awards this evening, congratulations to both of them! Sydney Gidabuday and his El Modena teammates show their support and solidarity.  SOURCE: Helen Moreno in California.