AJALI BARABARANI: Rage apata ajali ya gari
MWENYEKITI wa Simba aliyemaliza muda wake, Ismail Aden Rage, jana amenusurika kifo baada ya kupata ajali ya agari eneo Chigongwe, nje kidogo ya Manispaa ya Dodoma, wakati akiingia mjini humo kwa ajili ya kuhudhuria vikao vya Bunge Maalum la Katiba linaloanza leo. Kwa mujibu wa taarifa zilizolifikia Tanzania Daima wakati likienda mitamboni, zilisema kuwa Rage amelazwa katika Hospitali ya Rufaa ya mkoa wa Dodoma, akiwa na majeraha aliyoyapata yeye na watu wengine alioongozana nao katika gari moja. Saa chache kabla ya ajali hiyo, Rage alizungumza na Tanzania Daima na kuuushangaa uongozi mpya wa klabu ya Simba chini ya Rais Evans Aveva kwa taarifa yake kuwa umerithishwa deni la sh. mil. 250 na kuutaka kulitolea ufafanuzi, huku yeye akiahidi kuongea na wanahabari kuzungumzia sakata hilo. Aveva, juzi alibainisha kuwa uongozi wake unakabiliwa na changamoto nzito ya uendeshaji, baada ya kurithi deni hilo, huku wakiachiwa akaunti tupu. Alisema walichokuta ni sh.