Glasgow: Michezo ya Madola yamalizika
England waongoza, Kenya nao watamba; Mataifa madogo kabisa yaizidi Tanzania Michezo ya Jumuiya ya Madola iliyomalizika jijini Glasgow, Uskochi imemalizika kwa England kuibuka kidedea, wakizoa jumla ya medali 174, wakifuatiwa an Australia na Canada. Baada ya siku 11 zilizokutanisha wanamichezo mbalimbali kwenye michezo tofauti 17, pazia lilishushwa Hampden Park huku wenyeji wakishika nafasi ya nne, ambayo kwa udogo kijiografia si haba. Ofisa Mtendaji Mkuu wa Shirikisho la Michezo ya Jumuiya ya Madola, Mike Hooper alisema kwamba michezo hii ndiyo iliyofana zaidi katika miaka 84 ya historia yake. Scotland walipata medali 19 za dhahabu, idadi ambayo hawakupata kutwaa katika mashindano mengine. Kwa mara ya kwanza katika kipindi cha miaka 28, England walishika usukani kwa medali 58 za dhahabu, 59 za fedha na 57 za shaba. Australia walinyakua 49 za dhahabu, 42 za fedha na 46 za shaba huku Canada wakiwa na 32 za dhahabu, 16 za fedha na 34 za shaba. Nafasi ya tano i