Tathmini ya Madola, ifanyiwe kazi
Timu ya Tanzania kwenye michezo ya Jumuiya ya Madola yakaribishwa rasmi leo katika kijiji maalum cha michezo hiyo Glasgow Kwa mara ya kwanza katika historia ya Tanzania, Serikali ilikutana na wanamichezo kwa ajili ya kufanya tathmini ya ushiriki wa taifa kwenye michezo ya Jumuiya ya Madola ya 2014 ambayo Tanzania ilitoka kapa kwa mara ya pili mfululizo. Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe ndiye alikuwa mgeni rasmi katika tathmini hiyo iliyowahusisha wachezaji, makocha na viongozi wa vyama mbalimbali vya michezo. Katika tathmini hiyo, vyama vililalamikiwa kutokuwa makini katika kuziandaa timu zao kwa ajili ya mashindano ya kimataifa. Maandalizi duni ilikuwa ni moja ya sababu kubwa iliyotajwa katika tathmini hiyo iliyohusisha wanamichezo wa ngumi, riadha, mpira wa meza, judo, kuogelea, baiskeli na kunyanyua vitu vizito walioiwakilisha nchi katika michezo ya madola iliyofanyika Scotland. Maandalizi ya zimamoto ni ugonjwa sugu ulio kw