PHAUSTIN BAHA SULLE: MWANARIADHA ALIYEKATAA KUPOKEA ZAWADI BILA BENDERA YA NCHI YAKE KUPEPEA MBELE YAKE AKIWA VERACRUZ MEXICO
Mwanzo wa mashindano ya dunia mjini Veracruz Mexico, Tanzania ilipata medali ya Fedha kupitia mwanariadha Phaustin Baha Sulle Ilikuwa katika mbio za Lisbon Half Marathon 2000 ambapo wanariadha kutoka Kenya, Ethiopia, Moroco, Tanzania, Ulaya, Marekani na Asia walipokutana nchini Ureno kushiriki mashindano hayo makubwa duniani. Phaustin Sulle nyuma ya Paul Tergat Paul Tergat wa Kenya aliyekuwa akishikilia rekodi ya dunia ya nusu marathon kwa wakati huo alikuwepo katika mstari wa kuanzia mbio. Wanariadha wote walikuwa wakimtazama Tergat na wakenya wenzake, hawakujua kuna kijana chipukizi kutoka Babati Tanzania ambaye hakujali nani yupo, yeye alisubiri kwa hamu mbio zianze. Muda mfupi baadaye Paul Tergat alijikuta akitolewa jasho na Phaustin Baha Sulle kuanzia kilomita ya kwanza hadi ya kumi. Ndipo sasa Tergat alipotumia uzoefu wake kumdhibiti Sulle hatimaye Tergat alishinda mbio hizo kwa umbali mdogo sana kati yake na Phaustin Baha Sulle. Tergat alikimbia daki...