Jamali Malinzi, wadau kumlipa Kim
Jamali Malinzi Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Jamal Malinzi jana alitangaza rasmi kuondolewa kwa kocha Kim Poulsen, lakini akashindwa kueleza sababu za kuachana na mwalimu huyo kutoka Denmark. Malinzi, ambaye uongozi wake ulifanya kituo cha kuteua wachezaji wa timu ya taifa badala ya kazi hiyo kufanywa na kocha, pia jana aliongeza alitangaza kuwa fidia ya kuvunjwa kwa mkataba wa Poulsen zitalipwa kwa ushirikiano baina ya TFF na wadao, ambao pia hakuwataja. Poulsen, ambaye analipwa mshahara na serikali kutokana na ahadi ya Rais Jakaya Kikwete, ana mkataba unaoisha Mei mwakani na alipewa kazi hiyo baada ya kuonyesha mafanikio kwenye timu za vijana. Hivyo, kuvunjwa kwa mkataba huo kutalifanya Shirikisho hilo limlipe Poulsen mishahara yake ya miezi sita kulingana na mkataba wake. “Jukumu la kulipa gharama za kuvunja mkataba zitabebwa na TFF na baadhi ya wadau wa soka watatusaidia nusu ...