Training Center: Tanzania inahitaji kituo kikukwa cha michezo yote
Zambia Olympic Youth Development Center Mwaka 2004 Tanzania ilipata bahati ya kuahidiwa kujengewa kituo kikubwa cha kisasa cha michezo ( Tanzania Olympic Youth Development Center ) ambayo ingegharimu USD 10million lakini viongozi wa TOC kwa kushirikiana na viongozi wasio wazalendo walikwamisha. Kilichotakiwa na IOC ni kuhakikishiwa kwamba eneo kubwa lisilo na utata wa kisheria linapatikana ikiwa na vithibitisho vya kiumiliki ili hapo baadaye kusiwepo na utata ( contradiction ) za kisheria. Bila aibu wala uzalendo kamati ya Olimpiki Tanzania (TOC) ilihakikisha kwamba kituo hicho hakijengwi kwa sababu ya wao kuhofia masilahi yao ya upatikanaji wa tenda za kimichezo katika center zao walizojiwekezea. Kwa mfano: kama mtu anapata tenda ya Copa Coca-Cola ya Tsh: Bilioni kila mwaka alafu atawezaje kupata kiasi hicho cha pesa iwapo taifa litakuwa na center yake? Hivyo kigogo mmoja tu mwenye center yake alishawishi kamati nzima waikatae ofa hiyo ya IOC nao kwa...