Posts

Historia: Rais Jakaya Kikwete kufungua rasmi bunge la katiba leo

Image
RAIS Jakaya Kikwete ana siri nzito moyoni ya kile anachotaka kuwaambia Watanzania wakati atakapolihutubia Bunge Maalumu la Katiba leo mjini Dodoma. Hotuba hiyo inayoashiria uzinduzi rasmi wa Bunge hilo la kihistoria, inasubiriwa kwa hamu kubwa na Watanzania wote leo ambao watalazimika kusimamisha shughuli zao kwa takribani saa tatu kumsikiliza Rais Kikwete. Hamu ya hotuba ya Rais Kikwete inatokana na hotuba ya Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Jaji Joseph Warioba, aliyechambua hoja baada ya hoja kuonyesha kwamba Muungano wa Tanzania wa serikali mbili ulioachwa na waasisi, haupo tena licha ya shinikizo la Chama Cha Mapinduzi (CCM), kutaka kuendelea na serikali mbili.

UTAIFA KWANZA: Holili yadhamini Sokoine Mini Marathon

Image
KLABU ya Holili Youth Athletic Club (HYAC) ya mjini Holili, mkoani Kilimanjaro, imejitosa kudhamini mbio za Sokoine Mini Marathon zinazotarajiwa kufanyika Aprili 12, mwaka huu katika Kijiji cha Monduli Juu, Wilaya ya Monduli, mkoani Arusha. Katika udhamini huo, HYAC imetoa sh milioni moja zitakazotumika kuchapisha namba (Bibs), 1,000 za utambulisho za wanariadha. Akizungumza na Tanzania Daima jana, Mkurugenzi wa HYAC, Domician Genandi, alisema kilichomsukuma kufanya hivyo ni moyo wa uanamichezo na kuongeza kuwa, kwa mwaka huu wamedhamiria kuongeza nguvu zote kuinua mchezo wa Riadha nchini. “Nimeamua kusaidia nikiwa kama mdau, sababu lengo letu ni kuendeleza michezo Tanzania, sisi wadau tunatakiwa tuwe na mtazamo wa ushindi kama taifa na si ushindi wa klabu zetu binafsi tu, au wanariadha wetu tu, HYAC tunatambua jitihada binafsi zinazofanywa na waandaaji kumuenzi hayati Sokoine,” alisema Genandi. Aidha, Genandi alisema kwa mwaka huu k...

Holili athletes support Sokoine half marathon

Image
Mr. Domician Genand / Photo by Asili Yetu Tanzania  By Joseph Mchekadona 17th March 2014 Kilimanjaro-based Holili Youth Athletic Club yesterday donated 1,000 bibs to the forthcoming Edward Sokoine Mini Marathon which to be staged on April 12 in Monduli . The event is held to mark 30th anniversary since the death of the former prime minister. One of the organisers of the event Wilhelm Gidabuday thanked the athletics club for the donation describing it as timely and wisely. He said the bibs are good at any athletics event as they help to identify runners. Gidabuday also urged companies, organisations and individuals to emulate a good example set by the club “Bib numbers are good, it must be known that athletes at any event are known by bib numbers not names or faces. So as the organisers of the event we thank Holili Youth Athletic Club for this donation”, he said. On his remarks Holili Youth Athletic Club director Domician Genand said his club th...

Suleiman Nyambui: Tujitoe katika mashindano ya Jumuia za Madola

Image
Suleiman Nyambui Akizungumza na shirika la habari la BBC leo asubuhi Suleiman Nyambui alikiri Tanzania haina uwezo wa kupata medali hivyo ni bora tukajitoa kukwepa aibu. Nyambui amekaririwa akisema hivyo wakati siku chache zilizopia alikaririwa na Star Tv akijigamba kwamba sasa tutashinda medali baada ya kuwepo na taarifa kwamba timu za Tanzania zitapelekwa nchi za nje kufanya mazoezi kwa msaada wa waziri wa mambo ya nje na ushirikiano wa kimataifa Mheshimiwa Bernard Membe . Tuamini lipi kati ya maneno yaliyosemwa na mtu huyo huyo katika vyombo tofauti vya habari?

KIKATIBA YEYE NANI? Kibali ujenzi Yanga mwisho wa mwezi

Image
Mzee Ibrahim Akilimali WAKATI Wazee wa Klabu ya Yanga wakipiga mkwara wa kutaka ndani ya siku tano wawe wamepewa kibali cha ujenzi makao makuu ya klabu yao Jangwani, Halmashauri ya Ilala imesema jambo hilo litaanza kufanyiwa kazi mwishoni mwa mwezi huu. Juzi, Mwenyekiti wa Kamati ya Ujenzi ya Yanga, Francis Kifukwe, alilalamika kuwa, licha ya kutuma maombi muda mrefu Manispaa ya Ilala kuomba kibali cha ujenzi pamoja na kuongezewa eneo, lakini wahusika wamekuwa kimya na kibaya zaidi, waliwafukuza kwenye kikao cha juzi. Wakati Kifukwe akilalamika juzi, jana Katibu wa Baraza la Wazee wa Yanga, Ibrahim Akilimali, aliwaambia waandishi wa habari jijini Dar es Salaam kwamba, wanampa siku tano Meya wa Manispaa ya Ilala, Jerry Silaa, kuhakikisha wanatoa kibali kwa klabu hiyo kuanza ujenzi wa uwanja unaotarajiwa kuitwa ‘Jangwani City’. Akizungumza kwa mbwembwe, Akilimali alisema, wanatoa siku hizo kuhakikisha Silaa anatoa kibali, bila hivyo watahakikisha wanamwaga mboga, kwani ugali w...

CONVICTION: Bayern Munich President Uli Hoeness Sentenced to 3.5 Years in Prison

Image
The 1974 World Cup winner is said to have evaded €27.2 million in taxes and was lucky not to receive a five-year sentence, according to The Guardian 's Philip Oltermann : "The 62-year old asked for leniency having voluntarily disclosed his actions to authorities." Hoeness made well in excess of 200 appearances for Bayern across a nine-year spell with the club before heading to Nuremberg on loan. His crime is sure to dampen a fantastic legacy he has built at Bayern since retiring in 1979, an era that has seen the club rise to prominence with multiple domestic titles and European successes. Most recently, Bayern 's greatest achievement with Hoeness as president arrived in the form of a quintet-winning 2013. Hoeness had hoped to avoid a prison sentence after turning himself in last year, per The Associated Press (via The Guardian ). Upon coming clean, German chancellor Angela Merkel expressed her disappointment toward the Bayern president, as qu...

MUZIKI: GK atangaza ujio mpya wa East Coast Team

Image
MKALI wa muziki wa kizazi kipya nchini, Gwamaka Kaihula ‘King Crazy GK’ amewataka wapenzi wa kundi la muziki huo la East Coast Team kukaa mkao wa kula baada ya wasanii waliokuwa wanaunda kundi hilo kujipanga kurudi upya. Baadhi ya wasanii ambao walikuwa wanaunda kundi hilo ni Ambwene Yesaya ‘AY’, Hamis Mwinjuma ‘Mwana FA’, mwanadada Judith Wambura ‘Jide’ na GK. Akizungumza jijini Dar es Salaam jana, GK alisema, huu ni wakati wao wa kufanya kazi kama zamani kwa kutoa burudani nzuri ambazo zimekwenda shule. “Tumeanza kuongeza nguvu katika kundi letu jipya, tunatakiwa kufanya kitu kipya katika kiwango cha juu vitu ambavyo watu hawataamini kama ni sisi,  tunatakiwa kuwa katika viwango vingine kwasababu tukiwa katika hali ilele inamaana kutakuwa hakuna maana ya kurudi upya,” alisema GK. Alisema wameshapata studio ya kimataifa ambayo itatumika kutengenezea kazi zao, na kwamba kwasasa ataanza kutambulisha kazi yake ambayo ameshirikiana na AY na Mwana FA. GK alishawahi kut...