Tunasubiri ‘Matokeo Makubwa Sasa’
Safari hii, serikali kwa kutumia uhusiano wake wa kitamaduni na nchi za China, Uturuki, Ethiopia na New Zealand iliweza kutuma wanamichezo wake kwenye nchi hizo tofauti kulingana na mazingira mazuri ya mchezo fulani ili waweze kujiandaa ipasavyo. Tanzania ni miongoni mwa nchi ambazo bendera yake itapepea jijini Glasgow, Scotland katika ufunguzi wa Michezo ya Jumuiya ya Madola itakayofanyika Julai 23 kwenye Uwanja wa Celtic Perth. Michezo hiyo muhimu hushirikisha nchi wanachama wa jumuiya hiyo ambazo ziliwahi kuwa koloni la Uingereza na mwaka huu inatarajiwa kushirikisha mataifa 71 ambayo yatachuana katika michezo 17 tofauti itakayofikia tamati Agosti 3. Katika michezo hii Tanzania inatarajiwa kuwakilishwa na wanamasumbwi, wanariadha, kunyanyua vitu vizito, mpira wa meza, wachezaji judo, waendesha baiskeli na waogeleaji ambao tayari wameshawasili kwenye kijiji cha michezo nchini Scotland tayari kwa mi...