Wawakilishi Madola wameifedhehesha nchi
Julai 16, Rais Jakaya Kikwete alimkabidhi Bendera ya Taifa nahodha wa Tanzania katika Michezo ya Jumuiya ya Madola, Seleman Kidunda kwa matumani kwamba timu itaipeperusha vyema kwenye michezo hiyo ya 20 iliyofanyika kwenye jiji la Glasgow, Scotland. Rais alifika Uwanja wa Taifa kwa kazi hiyo, akiwa na matumaini ya vijana wake kuwa watalinda heshima ya nchi katika michezo hiyo mikubwa iliyoshirikisha mataifa 71. Kinyume na matarajio hayo, matokeo ndivyo kama yalivyosikika na kuonekana. Tanzania haikuambulia hata medali moja katika michezo hiyo ya Madola kama ilivyokuwa kwenye michezo ya 19 iliyofanyika New Delhi, India mwaka 2010. Katika michezo hii, tunautazama ushiriki wa Tanzania katika maeneo mawili; maandalizi na ushiriki wa timu zake saba za riadha, ngumi, kuogelea, mpira wa meza, judo, kunyanyua vitu vizito na baiskeli. Katika maandalizi, hakuna ubishi kuwa Tanzania ilivurunda. Viongozi waliosindikiza timu kwenye michezo ya Madola pamoja na watu wengine, ...