Posts

Wawakilishi Madola wameifedhehesha nchi

Image
Julai 16, Rais Jakaya Kikwete alimkabidhi Bendera ya Taifa nahodha wa Tanzania katika Michezo ya Jumuiya ya Madola, Seleman Kidunda kwa matumani kwamba timu itaipeperusha vyema kwenye michezo hiyo ya 20 iliyofanyika kwenye jiji la Glasgow, Scotland. Rais alifika Uwanja wa Taifa kwa kazi hiyo, akiwa na matumaini ya vijana wake kuwa watalinda heshima ya nchi katika michezo hiyo mikubwa iliyoshirikisha mataifa 71. Kinyume na matarajio hayo, matokeo ndivyo kama yalivyosikika na kuonekana. Tanzania haikuambulia hata medali moja katika michezo hiyo ya Madola kama ilivyokuwa kwenye michezo ya 19 iliyofanyika New Delhi, India mwaka 2010. Katika michezo hii, tunautazama ushiriki wa Tanzania katika maeneo mawili; maandalizi na ushiriki wa timu zake saba za riadha, ngumi, kuogelea, mpira wa meza, judo, kunyanyua vitu vizito na baiskeli. Katika maandalizi, hakuna ubishi kuwa Tanzania ilivurunda. Viongozi waliosindikiza timu kwenye michezo ya Madola pamoja na watu wengine, ...

Nanjing Youth Olympic Village Officially Opens

Image
Nanjing Youth Olympics Village opening ceremony [Photo: Imagine China] The Nanjing Youth Olympic Village has officially opened this Tuesday. The Olympic Village for the teenagers will accommodate about 6-thousand athletes, team officials, youth ambassadors and International Olympic Committee officials.  Executive President of the Nanjing 2014 organizing committee, Yang Weize, along with IOC Executive Director, Gilbert Felli, have attended the opening ceremony. The first batch of athletes arrived in Nanjing on Monday. The second route of the physical torch relay for this year's Youth Olympics was also completed this Tuesday. SOURCE: Xinxua

MICHEZO MADOLA: Makocha wajilipua

Image
Makocha wa timu za Tanzania zilizoshiriki na kufanya vibaya kwenye michezo ya Jumuiya ya Madola iliyomalizika nchini Scotland wamefunguka na kueleza masaibu yaliyozisibu timu zao. Katika kile kinachoonyesha kuwa kimya kingi kina mshindo, mkuu makocha hao wameeleza mambo mazito ambayo ni vigumu kuyaamini, lakini  ndiyo yaliyozikumba timu za Tanzania. Mojawapo ni jambo ambalo ni hatari kiafya, aibu na fedheha,  likiwamo la mabondia kulazimika kupokezana vikinga ulimi, hali inayoweza kusababisha maradhi. Mtaalam mmoja wa michezo, Dk Nassoro Matuzya alisema jana kuwa kubadilisha vikinga ulimi ni hatari na kiafya hairuhusiwi, kwani mdomo ni mojawapo ya sehemu zenye bakteria wengi katika mwili wa binadamu, jambo ambalo ni rahisi kuambukizana magonjwa. “Wanaofanya hivyo wanapaswa kuwa na wataalam wa afya ili wawashauri kuhusu madhara yanayoweza kuwapata wanamichezo kwa kupewa vitu kama hivyo,” alisema na kuongeza kuwa kama kuna timu imewahi kufanya hivyo, wac...

Tunasubiri aibu tena: Medali ngumu Olimpiki ya Vijana

Image
Kwa mazingira haya ya mazoezi Tanzania itasubiri sana ushindi wa kupata medali. Makocha wa timu za Tanzania kwenye Olimpiki ya Vijana, wamesema wana kibarua kigumu cha kuhakikisha wanarejea na medali kwenye michezo hiyo itakayoanza Jumamaosi nchini China. Msafara wa wachezaji wanne na viongozi watatu uliondoka jana jioni na ndege ya Shirika la Qatar, na utakwenda moja kwa moja jijini Nanjing inapofanyika michezo hiyo. Wakizungumza na gazeti hili kwa nyakati tofauti, kocha wa timu ya riadha, Mwinga Mwanjala na mwenzake wa timu ya kuogelea, Ally Hamis Bamba walisema wana kibarua kigumu kwenye mashindano hayo. “Tunakwenda kushindana, lengo letu ni kuhakikisha tunashinda, kila nchi inahitaji medali na wachezaji wetu pia wanahitaji medali, tuna kibarua kigumu cha kuhakikisha tunapambana ili kushinda,” alisema Bamba. Wakati kocha wa riadha, Mwinga Mwanjala akisema wanakwenda kwenye mashindano hayo kama washindani, hivyo wanaamini nafasi ya kushinda wanayo.“Bahati nzuri mi...

Sports experts blast AT over poor Glasgow show

Image
Tanzania’s Fabian Joseph (third left) competes in the men’s marathon at the 2014 Commonwealth Games in Glasgow, Scotland. He finished 11th. PHOTO| AFP.       Arusha. Former athletes and sports administrators have blasted Athletics Tanzania (AT) for the country’s poor show at the recently-ended Commonwealth Games in Glasgow, Scotland. “The team that represented us did not comprise the best performers of our time,” lamented Wilhelm Gidabuday, a former national athlete who ruled the marathon race in the 1990s while in the US. He told The Citizen on Sunday from Dar es Salaam that he was surprised by the way the athletes who eventually represented the country were picked for training because he knew they were not the best “and hardly met the qualification standards.” “The selection was only made on the table and not in the field. I have every reason to believe that the selection was based on friendship and relations and not on field perform...

Hali ya Rage yaimarika Aga Khan

Image
HALI ya aliyekuwa Mwenyekiti wa klabu ya Simba, Ismail Aden Rage, imezidi kuimarika ambapo kwa sasa amelazwa katika Hospitali ya Aga Khan, Dar es Salaam. Rage alipata ajali juzi mkoani Dodoma, akiwa pamoja na majeruhi wenzake wanne walilazwa katika hospitali ya mkoa huo kabla ya kuhamishiwa Aga Khan. Akizungumza Dar es Salaam jana akiwa hospitalini hapo, Rage alisema anaendelea vizuri ambapo kwa mujibu wa daktari alisema itamchukua wiki tatu kupona kabisa bega lake. “Nashukuru naendelea vizuri na naendelea kupata huduma, daktari ameniambia baada ya wiki tatu nitakuwa nimepona kabisa hivyo naendelea na matibabu,” alisema. Akizungumzia ajali hiyo, Rage alisema dereva wa gari lao alikuwa anataka kulipita lori  lakini ghafla dereva wa lori hilo akaingia katikati ya barabara. “Hata hivyo, tunamshukuru sana dereva wetu kwa kuwa alipoona hivyo, badala ya kuligonga lori aliamua kwenda pembeni ndipo gari letu liliporuka na kuingia kwenye korongo likapinduka,” alise...

KAULI YA NYAMBUI NI KIPIMO TOSHA CHA UDHAIFU WA UZALENDO WETU

Image
Suleiman Nyambui / Mtanzania asiyejali sheria wala uzalendo KATI ya vipindi vya michezo redioni ambavyo hunipita kwa nadra sana ni kile cha Radio One Stereo. Siku chache zilizopita, nilikuwa nikifuatilia namna Maulid Kitenge alivyokuwa akimhoji Katibu Mkuu wa Chama cha Riadha Tanzania (RT), Selemani Mujaya Nyambui. Kitenge alikuwa akitaka kujua sababu ya timu ya Tanzania iliyoshiriki michuano ya Jumuiya ya Madola kurejea nyumbani bila ya hata kipande cha medali. Nyambui ambaye katika sauti yake unaweza kubaini mengi, alizungumza mambo ya ajabu ambayo hauwezi kutarajia kiongozi au mwanamichezo mwenye sifa yake anaweza kuzungumzia. Mwanariadha huyo wa zamani ambaye unaweza kumwita ni kati ya mashujaa waliowahi kuchukua medali na kuileta nyumbani kupitia michuano ya Olimpiki, alikuwa akizungumza sawa na mtu aliyekuwa hayuko vizuri, labda kwa uchovu au ni yule asiyejali tu. Wakati Kitenge akieleza alitaka kujua kwa nini timu hiyo haikuleta medali, Nyambui hakufafanua lo...