Sports Diplomacy: Waziri Membe kupeleka wanariadha 40 nje ya nchi
Mhe. Bernard Membe Tanzania inaelekea kupata nafasi ya kupeleka timu ya riadha nchini China, Ethiopia na Uturuki kwa maandalizi ya kuwanoa vijana kwa mashindano ya madola na kwa msaada wa waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Mhe. Bernard Membe. RT imeonyesha dalili za kuchagua wanariadha mezani badala ya mashindano ya wazi ili kufanya mchujo wa kidemokrasia. Mfumo ambao nchi za wenzetu kama Kenya wanafanya ili kuepusha upendeleo wa aina yoyote. Katibu wa RT Sulemain Nyambui amekaririwa na vyombo vya habari akidai kupeleka majina kwa waziri Membe. 'Wazalendo na wapenda haki tunadhani ipo haja ya kuandaliwa mashindano maalum yatakayopewa viwango kadha ambayo wakimbiaji wakifikia ndio wachaguliwe kwa uwazi badala ya kumpa mwanya kiongozi moja kumpendelea ndugu ama jamaa yake' Kuna tetesi kwamba kuna vijana na makocha ambao wamehakikishiwa safari hizo kwa ahadi maalum kwamba wakijiandaa kutoa chochote watahakikishiwa wanasafiri bila kujali uwezo