Fabian Joseph, Jackline Sekilu mabingwa Sokoine Min Marathon 2014
BINGWA wa mbio za Edmund World Half Marathon nchini Canada mwaka 2005, Fabian Joseph, na bingwa wa Kili Marathon 2014 kwa wanawake, Jackline Sekilu, wameibuka washindi wa Sokoine Min Marathon 2014, katika mashindano ya Kumbukumbu ya Miaka 30 ya kifo cha aliyekuwa Waziri Mkuu wa Tanzania, hayati Edward Moringe Sokoine, yaliyofanyika jana mjini hapa. Fabian aliibuka mshindi wa kwanza wa mbio hizo za kilometa 10 kwa kutumia dakika 34:28:04 na kufuatiwa kwa karibu na Alphonce Frank wa Shule ya Winning Spirit aliyetumia dakika 34:41:89 na nafasi ya tatu ikiangukia kwa mwanariadha Dickson Marwa wa Holili, aliyetumia dakika 34:57:47. Kwa kuibuka kidedea, Fabiani amezawadiwa fedha taslimu shilingi 500,000, kombe, medali na cheti maalum, wakati mshindi wa pili akipata shilingi 400,000, medali na cheti, huku mshindi wa tatu akipata shilingi 300,000, medali na cheti. Wanariadha wengine waliomaliza katika kumi bora na timu zao kwenye mabano ni Gabriel Gerald (Wining Spirit