Viongozi wa michezo nchini ‘janga la Taifa’
Mhe.Dr.Fenella Mukangara / Waziri wa Michezo Wakati wa utawala wa Baba wa Taifa, Marehemu Julius Kambarage Nyerere, Tanzania iliingia kwenye rekodi ya mataifa tishio barani Afrika katika michezo. Wakati huo, wanamichezo wa taifa waliaminika kwa Watanzania kila waliposema wanakwenda kushindana nje ya nchi. Si kama Tanzania ilishushiwa muujiza bali ilitokana na namna viongozi wa Serikali na wale wa michezo wa wakati huo walivyotambua wajibu wao. Historia zinaonyesha namna michezo ilivyofanyika kwa mpangilio kuanzia ngazi za shule, kata, wilaya, mkoa na taifa, vipaji vilionekana na Taifa likafanya vizuri kimataifa. Tanzania iling’ara kwenye mashindano ya Olimpiki, Jumuiya ya Madola na Afrika wakati huo kutokana na namna taifa lilivyotengeneza timu za ushindani kuanzia ngazi ya wilaya, mikoa na hata taifa hivyo kuwa na akiba ya vijana wengi wenye vipaji vya michezo. Tofauti na sasa ambapo kadri siku zinavyozidi kwenda ndivyo jahazi la michezo ya Tanzania linazidi ku