Hatimaye RT wakabwa mahakamani kwa madai ya Milioni 20
Suleiman Nyambui / Katibu mkuu wa Chama Cha Riadha Tanzania Kampuni ya SYMAITON SAPALI & CATHY CATERING imewaburuza viongozi wa Chama Cha Riadha Tanzania RT kwa deni la Tsh: 20,000,000 iliyotokana na chakula cha wanariadha wakati wa mashindano ya taifa yaliyofanyika Dar Es Salaam September 2012. Kesi hiyo (Civil Case Number 9/2014) ilifunguliwa katika mahakama ya wilaya ya Temeke siku za nyuma huku viongozi wa RT wakikaidi wito wa mahakama. Juzi (September 11, 2014) Katibu wa RT Suleiman Nyambui alihudhuria kesi hiyo baada ya mahakama kutoa amri kali ambapo angedharau amri hiyo huenda angekamatwa na kutiwa ndani. Akihojiwa na kituo kimoja cha redio hapo jana, Nyambui alikana kesi hiyo yenye kutia doa chama cha riadha, lakini muda mfupi baadae mwanasheria wa RT Thabit Bashir alithibitisha kuwepo kwa kesi hiyo. Hivi karibuni Suleiman Nyambui amekuwa akiandamwa kote kote hadi kutiliwa shaka katika biashara ya madawa ya kulevya! Akisthibitisha yey...