Uzembe waitoa Tanzania michezo ya Olimpiki 2016
Tanzania haitashiriki michezo ya soka kimataifa hadi mwaka 2016 kutokana na timu yake ya vijana wa umri chini ya miaka 23 kutoshiriki michuano ya kusaka tiketi ya kushiriki Olimpiki msimu wa 2015/2016. Kukosekana kwa timu hiyo ya U-23 kunaweza kuwa uzembe wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF). Katika ratiba iliyotolewa juzi na Shirikisho la Soka Afrika (CAF), pazia la michuano hiyo litafunguliwa Desemba. Katika michuano hiyo, raundi ya kwanza Rwanda itaanza kukata utepe kwa kumenyana na Somalia wakati Kenya itacheza na Zambia au Botswana. Kikosi hicho mara ya mwisho kilishiriki michezo ya Afrika mwaka 2011, kikiwa chini ya Jamhuri Kihwelo ‘Julio’ na kiliondolewa mapema kwenye michuano hiyo na Nigeria. Hata hivyo, U-23 haitashiriki michuano hiyo kwa vile Tanzania haikuthibitisha ushiriki wake huku viongoz...