KATIBA YA RT ILIYO KWAMA NA ATHARI ZAKE: NI JINSI GANI TAIFA LINGEHUJUMIWA; PONGEZI KWA USIKIVU WA BMT NA DEONIZ MALINZI
M/Kiti w BMT Deoniz Malinzi Hivi karibuni viongozi wa Chama Cha Riadha nchini (RT) walijaribu kwa njia zote 'hops and hooks' kupitisha katiba ambayo ingebeba masilahi yao binafsi na siyo masilahi ya taifa la Tanzania. Hata hivyo harakati za wadau wenye taaluma na uzoefu mkubwa wa mchezo wa riadha uliweza kuweka "STOP" katika jitihada hizo zilizovaliwa njuga na baadhi ya viongozi wa RT ambao waliwekwa na TOC na hadi sasa viongozi hao wachache wa juu wa RT bado wanatembelea viatu vya TOC. Deoniz Malinzi: Mwenyekiti wa Baraza la Michezo Tanzania (BMT) alitekeleza wajibu wake vizuri kwa kusikia vilio vya wadau, hatimaye aliangaza macho kupitia rasimu hiyo iliyojaa mbegu za 'ubinafsi' na kuamua kuzuia sheria hiyo isipitishwe hadi marekebisho kadhaa ifanyike. 'Hongera mzee Malinzi' kwa kujali haki na usawa ambao ndiyo chimbuko la amani na ustawi wa jamii na taifa letu la Tanzania. Vipengele vya kijambazi katika rasimu: Mtanzania anayehubiriwa ...