Posts

KATIBA YA RT ILIYO KWAMA NA ATHARI ZAKE: NI JINSI GANI TAIFA LINGEHUJUMIWA; PONGEZI KWA USIKIVU WA BMT NA DEONIZ MALINZI

Image
M/Kiti w BMT Deoniz Malinzi Hivi karibuni viongozi wa Chama Cha Riadha nchini (RT) walijaribu kwa njia zote 'hops and hooks' kupitisha katiba ambayo ingebeba masilahi yao binafsi na siyo masilahi ya taifa la Tanzania. Hata hivyo harakati za wadau wenye taaluma na uzoefu mkubwa wa mchezo wa riadha uliweza kuweka "STOP" katika jitihada hizo zilizovaliwa njuga na baadhi ya viongozi wa RT ambao waliwekwa na TOC na hadi sasa viongozi hao wachache wa juu wa RT bado wanatembelea viatu vya TOC. Deoniz Malinzi: Mwenyekiti wa Baraza la Michezo Tanzania (BMT) alitekeleza wajibu wake vizuri kwa kusikia vilio vya wadau, hatimaye aliangaza macho kupitia rasimu hiyo iliyojaa mbegu za 'ubinafsi' na kuamua kuzuia sheria hiyo isipitishwe hadi marekebisho kadhaa ifanyike. 'Hongera mzee Malinzi' kwa kujali haki na usawa ambao ndiyo chimbuko la amani na ustawi wa jamii na taifa letu la Tanzania. Vipengele vya kijambazi katika rasimu: Mtanzania anayehubiriwa

WIZARA YA MICHEZO INASTAHILI KUWAJIBIKA KWA NANI?; VYAMA VYA MICHEZO AMA TAASISI ISIYO YA KISERIKALI?

Image
FABRIZIO CALDARONE LEONARD THADEO Hivi karibuni Chama Cha Tennis Tanzania (Tanzania Tennis Association) kilipitisha katiba yake na kufanya uchaguzi mkuu wa kuchagua viongozi wake baada ya miaka mingi ya udikteta ndani ya chama hicho. Hata hivyo baada ya muda mfupi wa furaha kwa wapenzi na wadau wa mchezo huo nchini, mzimu wa uongozi wa zamani umeendelea kuikumba taasisi hiyo muhimu katika michezo. Katibu wa zamani (aliyelazimika kujiuzulu ) INGER NJAU na mwenzake FABRIZIO CALDARONE wamekuja na taasisi yao mpya ya ATP TENNIS FOR CHARITY ambapo huko ulaya kuna taasisi inayofahamika kwa jina la TENNIS FOR AFRICA , “ taasisi hizo mbili zenye majina tofauti lakini zenye wanachama haohao ( Inger Njau na Fabrizio Caldarone ) zina harufu ya utata” alisema mjumbe moja ambaye hakupenda jina lake litajwe. “Lakini utata zaidi ni pale ambapo mkurugenzi wa michezo nchini LEONARD THADEO alipowapa kibali cha kuendesha "shughuli za Tennis" kwa viongozi hao wa kigeni na

PONGEZI: WAJUMBE WA (RT) WAKATAA MJADALA WA KATIBA HADI WADAU WOTE WAPATE FURSA YA KUIPITIA; TOFAUTI NA MATAKWA YA VIONGOZI

Image
Wanariadha wa kimataifa wa Tanzania Morogoro Leo Agosti 25, 2013 ilikuwa siku ya kujadiliwa na kupitishwa kwa katiba mpya ya Chama cha Riadha Tanzania (RT), hata hivyo kwa mara ya kwanza viongozi wenye nyuso za kuogopwa na wajumbe kutoka mikoani hawakuamini macho yao pale ambapo walishuhudia upinzani mkali wenye kuambatana na maswali yaliyoenda shule kutoka kwa wajumbe wa mkutano mkuu kutoka mikoa yote ya Tanzania Bara. Mjadala huo mzito ulianza pale ambapo baadhi ya wajumbe walidai kupewa 'hadidu rejea' kabla ya ajenda kuu kuanza, wengine walihoji vyema kabisa kwamba "huu ni mjadala wa katiba mpya au ni mjadala wa mabadiliko ya katiba"?. Mara ghafla viongozi hao wa RT waliozoea kubebwa ba viongozi wa TOC ambao wameegemea pande zote (RT na TOC) kwa uroho wa kimasilahi, walijikuta wakiwa hawana pa kuegemea kutokana na moto mkali kutoka mikoani. Baada ya mabishano yaliyoambatana na 'Cross Examination' RT na ndugu zao TOC hawakuwa na namna nyingine ba

JUMA IKANGAA: “The will to win is nothing without the will to prepare”

Image
Juma Ikangaa   Juma Ikangaa ni kati ya wanariadha wachache sana duniani waliodhaminiwa na kampuni moja ya viatu kuanzia mwanzo wa harakati zake za riadha hadi kustaafu kwake bila kuhama hama kimasilahi. Nchini Japan Juma Ikangaa anafahamika kuliko hata viongozi wakubwa wa nchi kutokana na uaminifu mkubwa aliouwekeza wakati akishiriki riadha chini ya udhamini wa kampuni ya vifaa vya michezo ya ASICS ya Japan . Mwaka 1984 katika Olimpiki ya Los Angeles California , kwa heshima ya Juma Ikangaa, kampuni ya vifaa vya ASICS ya Japan iliipatia timu ya Tanzania vifaa vyote kwa timu nzima ya Tanzania, kati ya vifaa vingi vilivyotolewa na kampuni hiyo ni pamoja na (track suits 1,000) ambazo kwa sasa Riadha Tanzania haiwezi kupata kutokana na sura mbaya iliyojengeka baada ya makampuni mawili ya PUMA na LINING kuhujumiwa na viongozi wa RT na TOC ambao baadhi yao hadi sasa wapo katika uongozi wa vyama hivyo. 'Ndiyo maana hata leo huko Morogoro wanariadha chipukizi wanakimbia peku hali mak

KAMANDA (RT) ATOKA NDUKI MOSCOW, ASEMA “TUMESHINDWA”

Image
Rais wa chama cha riadha Tanzania (RT) Anthony Mtaka amerejea Tanzania wakati wanariadha wawili wakiwasili Moscow tayari kwa mashindano. Kiongozi huyo aliyetangulia siku kadhaa kabla ya wachezaji amerudi akiwa na hasira isiyo na kifani, akizilaumu vyombo vya habari kwa kile alichodai kwamba “wanahabari wanawasikiliza watembea miguu wasio na tija katika mchezo wa riadha na kuwaacha wao wenye akili zao”. Pia alinukuliwa akimwaga lawama kwa makampuni ya kitanzania kwa kukataa kudhamini chama cha riadha. “Tumeandika maandiko mengi kwa robo tatu ya makampuni nchini, lakini hamna hata kampuni moja iliyokubali” alihoji Mtaka wakati akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar Es Salaam jana. Sababu ya makampuni kukataa: Wakurugenzi wa makampuni wanajali sheria ambapo kabla ya kuidhinisha udhamini katika taasisi yoyote,  ‘ cross checks na double checks’ hufanyika kwanza, ambapo kasoro zikipatikana udhamini hautolewi.   Chama cha Riadha hakikufuata katiba wakati wa uchaguzi mk

Mo Farah reaches World 5,000m final to keep alive double hopes

Image
Mo Farah's bid to add the World 10,000m and 5,000m titles to his Olympic golds remains on track after he eased into the final over the shorter distance. The defending champion was fifth in his heat, the final automatic qualifying position, in 13 minutes 23.93 seconds. If he wins Friday's final, Farah will emulate Ethiopia's Kenenisa Bekele and become the second man to win 10,000m and 5,000m Olympic and World titles. "You have to do the job without going crazy," the Briton told BBC Sport.  "My body feels good, the team have been looking after me well and I'm recovering well." The 30-year-old, who won the distance double at the London 2012 Olympics, became the first British man to win a 10,000m world title last Saturday. And he began his defence of the 5,000m crown he won in Daegu in 2011 in comfortable fashion. He was in third or fourth for much of the heat befor

BARUA YA WAZI KUTOKA KWA MWANARIADHA WA ZAMANI WA TANZANIA

Image
Wazee, Nakumbuka sana wakati nilikuwa nasoma Kibasila Secondary School pale Chang'ombe karibu na uwanja wa chuma yaani uwanja wa taifa, kila mara nikitoka shuleni nilikuwa napita pale uwanjani ili nikawaone wanariadha wa timu ya JWTZ na JKT wakifanya mazoezi ya uwanjani. Nawakumbuka wakina Gwangwai, Kijuu, Ndemandio, Francis John na wengineo ambao walikuwa wakifanya mazoezi ya mbio za mita 10,000, walikuwa wakipiga mita 400x20 wanapunzika kwa kujogi mita 200 na walikuwa wakizipiga sekunde 60 kila moja na mbili za mwisho walikuwa wakizipiga kwa sekunde 56. Upande mwingine walikuwa Musa Luliga, Kijuu na Marwa kwa jina jingine Alberto Juantorena wanapiga mita 300x15 walikuwa wanazipiga kwa sekunde 36 na ya mwisho wanaileta kwa sekunde 34. Hawa jamaa zetu walikuwa hawapati mialiko tuu, wao walikuwa wanasubiri michezo ya majeshi, nina hakika kama wangepewa nafasi ya kwenda Oslo, Berlin au Stockholm Grand Prix wangefanya maajabu kabisa. Jamani tuwakumbuke hawa ndu