Posts

Showing posts with the label Michezo

Thadeo calls for fair refereeing

Image
National Director of Sports Leonard Thadeo presents Asma Shafi with a certificate for taking part in a five-day Copa Coca-Cola referees and coaches course at the National Stadium in Dar es Salaam over the weekend. Photo | Michael Matemanga   The National Director of Sports, Leonard Thadeo, has exhorted football referees in the country to observe fair play and abide by the laws of the game while officiating matches at various tournaments. Thadeo made the call during the official closing of a five-day referees and coaches course for the forthcoming U15 Copa Coca-Cola tournament at the National Stadium over the weekend. He said that in recent years there has been an outcry on biased refereeing and challenged the referees to live up to the public expectations of advocating ‘nothing else but fair decisions’. “After all, this is a career you have chosen to earn your living from and we don’t expect you to be lured by gifts or money at the expense of jeopardising your career,”

Tufanye sensa ya vyama vya michezo nchini

Image
Dioniz Malinzi / Bosi wa Baraza la Michezo Tanzania Mwaka 2014 unakaribia kumalizika. Ni dhahiri hali ni mbaya katika medani ya michezo nchini na hiyo ni kutokana na matokeo tuliyoona kwa timu na wanamichezo wetu. Kimsingi, Tanzania imeharibu na kutia aibu kuanzia soka, ambayo ndiyo mchezo maarufu, hadi michezo mingine. Viongozi wenye dhamana katika michezo na wao wanaingiza siasa badala ya kuangalia nini wajibu wao na kwa chama na manufaa ya taifa. Tumewahi kupiga kelele sana katika eneo la michezo kuwa udhaifu wa uongozi na hasa kwa kutokuwa na dhamira na dira ya maendeleo, ndiyo kunachangia kutopiga hatua. Kuvurunda kwa wanamichezo wa Tanzania katika mashindano mbalimbali, kutokana na kukosa umakini na zaidi ni udhaifu wa uongozi katika vyama na klabu. Kwa jinsi hiyo, itachukua muda mrefu Tanzania kupiga hatua katika michezo kama mfumo wa utendaji ndani ya vyama hautabadilika. Kutokana na msingi huo, kuna haja kwa mamlaka inayohusika na michezo yote kufany

Okwi arejea Simba

Image
Emmanuel Okwi /Mchezaji maarufu wa soka HATIMAYE mshambuliaji wa kimataifa wa Uganda, Emmanuel Okwi, jana amesaini kuichezea klabu yake ya zamani ya Simba kwa mkataba wa miaka miwili. Habari zilizopatikana jana jioni, zilisema nyota huyo ambaye hatima yake ndani ya klabu ya Yanga ilikuwa gumzo kubwa, jana alitarajiwa kusaini mkakaba huo kuwatumikia Wekundu wa Msimbazi kwa kipindi kingine. Kurejea kwa Okwi Msimbazi, kunamweka katika wakati mgumu mchezaji Benard Musoti, nyota wa kimataifa wa Kenya, kwani sasa ni yeye sasa anayechungulia dirisha la kutokea, ama Pierre Kwizera. Okwi kutua Simba, ni kama kurejea nyumbani kwani ndio klabu aliyojiunga nayo kwa mara ya kwanza nchini akitokea Uganda na kung’ara nayo, kabla ya kuihama na kujiunga Etoile du Sahel ya Tunisia na kisha Yanga. Sheria za usajili za Ligi Kuu Tanzania Bara zinataka klabu kuwa na nyota wa kigeni wasiozidi watano na mbali ya Okwi, nyota wengine wa kimataifa katika kikosi cha Simba ni, Raphael Kiongera, Joseph O

Michezo: Tufanye yafuatayo ili tusonge mbele

Image
Bernard Membe/Waziri mambo ya Nje Viongozi wa vyama vya michezo wanapaswa kurejesha serikalini ripoti ya jinsi maandalizi, safari na mashindano yalivyofanyika wakati wa mashindano ya Glasgow. Itakuwa ni kosa kubwa iwapo vyama vya michezo vitakabidhi ripoti zao kwa mkurugenzi wa michezo, badala yake viongozi wa vyama wakabidhi wenyewe. Pia itakuwa ni haki kabisa wataalamu wa michezo husika kushirikishwa siku ya ripoti hiyo kuwasilishwa ili nao watoe ushauri wao wa kitaalamu. Wachezaji walioshiriki pia wahusishwe ili waweze kusema yao ya mioyoni kwa uhuru na uwazi. ‘Hayo yakifanyika tutafanya vizuri safari ijayo kwani tutakuwa tumejua wapi tulijikwaa’

Bondia Mafuru akana kuugua tumbo Madola

Image
BAADA ya Shirikisho la Ngumi za Ridhaa Tanzania (BFT) kusema linaendelea na uchunguzi kubaini sababu iliyofanya bondia Nasser Mafuru ashindwe kupanda ulingoni, bondia huyo anawashangaa waliosema aliugua kwani alikuwa fiti kiafya. Mafuru hakupanda ulingoni katika mashindano ya Jumuiya ya Madola ambayo yalimalizila Agosti 3, huko Glasgow, Scotland kwasababu walizodai kwamba alishikwa na tumbo la kuharisha. Mafuru alisema kwa njia ya simu jana, kuwa alikuwa mzima na hajawahi kuumwa tangu walipofika katika mashindano hayo, na kwamba walichelewa kufika eneo ukumbini viongozi ambao aliongozana nao ndio waliotoa sababu za kuugua. “Mimi sikuugua nilikuwa mzima, lakini tulichelewa kufika ukumbini nilikuwa nishajiandaa baada ya kufika tukakuta wanamtangaza bingwa Yule ambaye nilitakiwa kucheza naye lakini nawashangaa waliosema kwamba nilikuwa naumwa wakati tulikuwa na daktari ambaye naye hakujua kuumwa kwangu,” alisema Mafuru. Aidha, Ma

Viongozi wa michezo nchini ‘janga la Taifa’

Image
Mhe.Dr.Fenella Mukangara / Waziri wa Michezo Wakati wa utawala wa Baba wa Taifa, Marehemu Julius Kambarage Nyerere, Tanzania iliingia kwenye rekodi ya mataifa tishio barani Afrika katika michezo. Wakati huo, wanamichezo wa taifa waliaminika kwa Watanzania kila waliposema wanakwenda kushindana nje ya nchi. Si kama Tanzania ilishushiwa muujiza bali ilitokana na namna viongozi wa Serikali na wale wa michezo wa wakati huo walivyotambua wajibu wao. Historia zinaonyesha namna michezo ilivyofanyika kwa mpangilio kuanzia ngazi za shule, kata, wilaya, mkoa na taifa, vipaji vilionekana na Taifa likafanya vizuri kimataifa. Tanzania iling’ara kwenye mashindano ya Olimpiki, Jumuiya ya Madola na Afrika wakati huo kutokana na namna taifa lilivyotengeneza timu za ushindani kuanzia ngazi ya wilaya, mikoa na hata taifa hivyo kuwa na akiba ya vijana wengi wenye vipaji vya michezo. Tofauti na sasa ambapo kadri siku zinavyozidi kwenda ndivyo jahazi la michezo ya Tanzania linazidi ku

Filbert Bayi aishangaa Serikali

Image
Katibu Mkuu wa Kamati ya Olimpiki Tanzania (TOC), Filbert Bayi amesema ripoti ya timu za Tanzania zilizoshiriki michezo ya Jumuiya ya Madola imekwama baada ya Serikali kutaka wanamichezo wote waliokwenda Scotland kuhusishwa wakati itakapowasilishwa kwao. Bayi alisema Serikali imetaka wachezaji walioshiriki kwenye michezo hiyo kuwepo wakati vyama vyao vikiwasilisha ripoti zao za Madola. “Ripoti zimechelewa kwa kuwa Serikali imetaka wanamichezo wote waliokuwa Scotland kuwapo katika kikao cha tathmini, hiyo ni gharama, hivyo tuko kwenye mchakato wa kutafuta fedha ili kufanikisha hilo,” alisema. Alisema gharama za kufanya tathmini hiyo ni Sh 8 milioni, ambazo pia zitatumika kuwagharamia wachezaji wa mikoani walioshiriki michezo hiyo kuja Dar es Salaam ili kushiriki katika tathmini hiyo. “Hii ni mara ya kwanza ripoti ya Madola na tathmini yake kufanyika kwa kushirikis

Stars legends ready for Real Madrid encounter

Image
(TFF) president Jamal Malinzi (L) looks on as former Real Madrid player Reuben De la Red, (3rd-R), exchanges note with TSN group managing director Farouk Baghoza in Dar es Salaam yesterday. Tanzania XI assistant head coach, Jamhuri Kihwelo, is confident that his squad will outshine Real Madrid legends on Saturday at the National Stadium. Speaking yesterday, Kihwelo said his team was physically fit and ready to take on the Real legends. The outspoken coach, who should also have played on Saturday, said only three players were missing from the camp while disclosing that goalkeepers, Mohamed Mwameja and Peter Manyika have already joined the team. According to him, the players, who hung their boots several years ago, are fit enough to play any top team after just a few days of training. He singled out Yusuf Macho, Abdul Maneno, Abdul Mashine, Said Maulid as among those who are still on top of their game. “We’re ready for them, I am sure that our legends will play

Lipumba: Tuwekeze katika michezo

Image
Ni ndoto kwa Tanzania kufanya vizuri kwenye michezo kitaifa na kimataifa bila kuwekeza kwenye kukuza vipaji vya vijana kama ambavyo zimefanya nchi nyingine duniani. Huo ni ushauri wa Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi (CUF), Profesa Ibrahim Lipumba katika mahojiano maalumu na gazeti hili mwishoni mwa wiki. Prof Lipumba, ambaye mbali ya kubobea katika uchumi na siasa, alisema Tanzania haina budi kuwekeza katika michezo kuanzia elimu ya awali, msingi, sekondari hadi vyuo vikuu ambako vipaji vipya vitaweza kuibuliwa. Alisema Tanzania imekuwa ikifanya vibaya kimichezo kutokana na watoto wake wengi kudumaa kimwili kutokana na lishe duni kwao na wazazi wao. “Tunafanya vibaya kimichezo, tunatafuta sababu, lakini sababu zipo katikati yetu,” alieleza Prof Lipumba na kuongeza kuwa asilimia 42 ya watoto nchini wamedumaa, jambo ambalo linawaathiri katika mambo mengi yakiwamo michezo. Msomi huyo ambaye ni shabiki wa klabu ya Simba alisema uwekezaji ambao umefanywa kwa mfano n

Ikangaa, Shahanga waishangaa RT

Image
Kanali Mstaafu Juma Ikangaa Bingwa wa Afrika wa 1982, Juma Ikangaa na mshindi wa medali fedha ya Jumuiya ya madola, Gidamis Shahanga wamelishangaa Shirikisho la Riadha Tanzania (RT) kushindwa kupeleka timu kwenye Mashindano ya Afrika yanayoendelea nchini Morocco. Wanariadha hao wakongwe wamesema kuwa, kati ya vioja vinavyofanywa na RT ni kushindwa kupeleka timu kwenye mashindano makubwa kama hayo na kusisitiza kuwa kutokwenda kwenye mashindano hayo kutaiweka Tanzania katika mazingira magumu  kwenye Michezo ya Afrika (All African Games) mwakani. Gidamis Shahanga Wakizungumza na gazeti hili kwa nyakati tofauti jana, walisema, Tanzania ilipaswa kutumia mashindano ya Afrika kuwapima wanariadha wake kwa maandalizi ya Michezo ya Afrika. “RT imekosea kutopeleka timu Morocco, tunaambiwa imepeleka wanariadha wawili ambao  wamekwenda kuiwakilisha Zanzibar na si Tanzania bara,” alisema Ikangaa aliyewahi kuwa bingwa wa marathoni kwenye mashindano hayo ya 1982, nchini Mi

Wawakilishi Madola wameifedhehesha nchi

Image
Julai 16, Rais Jakaya Kikwete alimkabidhi Bendera ya Taifa nahodha wa Tanzania katika Michezo ya Jumuiya ya Madola, Seleman Kidunda kwa matumani kwamba timu itaipeperusha vyema kwenye michezo hiyo ya 20 iliyofanyika kwenye jiji la Glasgow, Scotland. Rais alifika Uwanja wa Taifa kwa kazi hiyo, akiwa na matumaini ya vijana wake kuwa watalinda heshima ya nchi katika michezo hiyo mikubwa iliyoshirikisha mataifa 71. Kinyume na matarajio hayo, matokeo ndivyo kama yalivyosikika na kuonekana. Tanzania haikuambulia hata medali moja katika michezo hiyo ya Madola kama ilivyokuwa kwenye michezo ya 19 iliyofanyika New Delhi, India mwaka 2010. Katika michezo hii, tunautazama ushiriki wa Tanzania katika maeneo mawili; maandalizi na ushiriki wa timu zake saba za riadha, ngumi, kuogelea, mpira wa meza, judo, kunyanyua vitu vizito na baiskeli. Katika maandalizi, hakuna ubishi kuwa Tanzania ilivurunda. Viongozi waliosindikiza timu kwenye michezo ya Madola pamoja na watu wengine,

MICHEZO MADOLA: Makocha wajilipua

Image
Makocha wa timu za Tanzania zilizoshiriki na kufanya vibaya kwenye michezo ya Jumuiya ya Madola iliyomalizika nchini Scotland wamefunguka na kueleza masaibu yaliyozisibu timu zao. Katika kile kinachoonyesha kuwa kimya kingi kina mshindo, mkuu makocha hao wameeleza mambo mazito ambayo ni vigumu kuyaamini, lakini  ndiyo yaliyozikumba timu za Tanzania. Mojawapo ni jambo ambalo ni hatari kiafya, aibu na fedheha,  likiwamo la mabondia kulazimika kupokezana vikinga ulimi, hali inayoweza kusababisha maradhi. Mtaalam mmoja wa michezo, Dk Nassoro Matuzya alisema jana kuwa kubadilisha vikinga ulimi ni hatari na kiafya hairuhusiwi, kwani mdomo ni mojawapo ya sehemu zenye bakteria wengi katika mwili wa binadamu, jambo ambalo ni rahisi kuambukizana magonjwa. “Wanaofanya hivyo wanapaswa kuwa na wataalam wa afya ili wawashauri kuhusu madhara yanayoweza kuwapata wanamichezo kwa kupewa vitu kama hivyo,” alisema na kuongeza kuwa kama kuna timu imewahi kufanya hivyo, wachezaji wa

Tunasubiri aibu tena: Medali ngumu Olimpiki ya Vijana

Image
Kwa mazingira haya ya mazoezi Tanzania itasubiri sana ushindi wa kupata medali. Makocha wa timu za Tanzania kwenye Olimpiki ya Vijana, wamesema wana kibarua kigumu cha kuhakikisha wanarejea na medali kwenye michezo hiyo itakayoanza Jumamaosi nchini China. Msafara wa wachezaji wanne na viongozi watatu uliondoka jana jioni na ndege ya Shirika la Qatar, na utakwenda moja kwa moja jijini Nanjing inapofanyika michezo hiyo. Wakizungumza na gazeti hili kwa nyakati tofauti, kocha wa timu ya riadha, Mwinga Mwanjala na mwenzake wa timu ya kuogelea, Ally Hamis Bamba walisema wana kibarua kigumu kwenye mashindano hayo. “Tunakwenda kushindana, lengo letu ni kuhakikisha tunashinda, kila nchi inahitaji medali na wachezaji wetu pia wanahitaji medali, tuna kibarua kigumu cha kuhakikisha tunapambana ili kushinda,” alisema Bamba. Wakati kocha wa riadha, Mwinga Mwanjala akisema wanakwenda kwenye mashindano hayo kama washindani, hivyo wanaamini nafasi ya kushinda wanayo.“Bahati nzuri mi

KAULI YA NYAMBUI NI KIPIMO TOSHA CHA UDHAIFU WA UZALENDO WETU

Image
Suleiman Nyambui / Mtanzania asiyejali sheria wala uzalendo KATI ya vipindi vya michezo redioni ambavyo hunipita kwa nadra sana ni kile cha Radio One Stereo. Siku chache zilizopita, nilikuwa nikifuatilia namna Maulid Kitenge alivyokuwa akimhoji Katibu Mkuu wa Chama cha Riadha Tanzania (RT), Selemani Mujaya Nyambui. Kitenge alikuwa akitaka kujua sababu ya timu ya Tanzania iliyoshiriki michuano ya Jumuiya ya Madola kurejea nyumbani bila ya hata kipande cha medali. Nyambui ambaye katika sauti yake unaweza kubaini mengi, alizungumza mambo ya ajabu ambayo hauwezi kutarajia kiongozi au mwanamichezo mwenye sifa yake anaweza kuzungumzia. Mwanariadha huyo wa zamani ambaye unaweza kumwita ni kati ya mashujaa waliowahi kuchukua medali na kuileta nyumbani kupitia michuano ya Olimpiki, alikuwa akizungumza sawa na mtu aliyekuwa hayuko vizuri, labda kwa uchovu au ni yule asiyejali tu. Wakati Kitenge akieleza alitaka kujua kwa nini timu hiyo haikuleta medali, Nyambui hakufafanua lo

Glasgow: Michezo ya Madola yamalizika

Image
England waongoza, Kenya nao watamba; Mataifa madogo kabisa yaizidi Tanzania Michezo ya Jumuiya ya Madola iliyomalizika jijini Glasgow, Uskochi imemalizika kwa England kuibuka kidedea, wakizoa jumla ya medali 174, wakifuatiwa an Australia na Canada. Baada ya siku 11 zilizokutanisha wanamichezo mbalimbali kwenye michezo tofauti 17, pazia lilishushwa Hampden Park huku wenyeji wakishika nafasi ya nne, ambayo kwa udogo kijiografia si haba. Ofisa Mtendaji Mkuu wa Shirikisho la Michezo ya Jumuiya ya Madola, Mike Hooper alisema kwamba michezo hii ndiyo iliyofana zaidi katika miaka 84 ya historia yake. Scotland walipata medali 19 za dhahabu, idadi ambayo hawakupata kutwaa katika mashindano mengine. Kwa mara ya kwanza katika kipindi cha miaka 28, England walishika usukani kwa medali 58 za dhahabu, 59 za fedha na 57 za shaba. Australia walinyakua 49 za dhahabu, 42 za fedha na 46 za shaba huku Canada wakiwa na 32 za dhahabu, 16 za fedha na 34 za shaba.   Nafasi ya tano i