Posts

Showing posts with the label Michezo

Mwanamichezo ateuliwa Waziri Mkuu

Image
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa Rais John Pombe Magufuli leo amemteua waziri mkuu mpya ambaye amejinadi kama mwanamichezo. Kassim Majaliwa hii leo ameapishwa kuwa wazii mkuu baada ya kuteuliwa na rais hatimaye kupitishwa na bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuwa waziri mkuu mpya wa serikali ya awamu ya tano. “Mimi ni mwanamichezo, ni kati ya wakufunzi 27 wa TFF, nitamwelekeza rais amteue waziri wa michezo anayefaa kwani michezo itatutangaza kimataifa” Hayo ni baadhi ya maneno yake waziri mkuu mpya.

'Azam defence unsettled'

Image
Azam FC coach Joseph Omog Azam FC coach Joseph Omog has declared that his team had plenty of leakages in the defence line, resulting in easy scoring of goals by opponents. In an interview with the Guardian the coach said that due to the signing of new defender Serge Pascal Wawa from Ivory Coast it needs time for other defenders to be able to play with him. Omog said so after his team was thrown out in ongoing Mapinduzi Cup by Mtibwa Sugar in the quarter final on Thursday.  Three central defenders Said Morad, Aggrey Moris and David Mwatika were trying to cope with the new defender and that is what cost the team. “We are still looking for someone who will play with Wawa in central defending. We tried Moris and at another time Mwatika but still there is a lot of mistakes occurring between them. I am still working on it and they will cope with each other soon. “We want to have a strong team as we want to retain our league title and we have a tough tournament toward

Tathmini ya Madola, ifanyiwe kazi

Image
Timu ya Tanzania kwenye michezo ya Jumuiya ya Madola yakaribishwa rasmi leo katika kijiji maalum cha michezo hiyo Glasgow Kwa mara ya kwanza katika historia ya Tanzania, Serikali ilikutana na wanamichezo kwa ajili ya kufanya tathmini ya ushiriki wa taifa kwenye michezo ya Jumuiya ya Madola ya 2014 ambayo Tanzania ilitoka kapa kwa mara ya pili mfululizo. Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe ndiye alikuwa mgeni rasmi katika tathmini hiyo iliyowahusisha wachezaji, makocha na viongozi wa vyama mbalimbali vya michezo. Katika tathmini hiyo, vyama vililalamikiwa kutokuwa makini katika kuziandaa timu zao kwa ajili ya mashindano ya kimataifa. Maandalizi duni ilikuwa ni moja ya sababu kubwa iliyotajwa katika tathmini hiyo iliyohusisha wanamichezo wa ngumi, riadha, mpira wa meza, judo, kuogelea, baiskeli na kunyanyua vitu vizito walioiwakilisha nchi katika michezo ya madola iliyofanyika Scotland. Maandalizi ya zimamoto ni ugonjwa sugu ulio kw

Theresia Dismas: Mama jasiri aliyeiletea Tanzania medali ya kwanza 1965

Image
Katika medani ya kimichezo Tanzania, historia ya kuletwa medali ya kwanza katika mshindano ya kimataifa ilitekelezwa na mwanamama Theresia Dismas Watanzania hatukumjua na hata tukatabiri kwamba mama yetu Theresia Dismas hayupo duniani kama nilivyowahi kuandika katika blog hii.  Ukweli ni kwamba mtanzania wa kwanza kufungua pazia la medali yupo hai na kwamba watanzania tuanze juhudi za kumtambulisha kwa viongozi wakuu wa serikali. Nilipoandika story kuwa mwanamke ndiye aliyeleta medali wa kwanza wengi walistuka maana historia hii inayowainua wanawake ilifichwa kwa muda mrefu bila shaka kutaka kupotosha ukweli. Jana nimepigiwa simu toka Uingereza na mtoto wa Theresia Dismas akaniambia habari yote katika blog yangu ni kweli “Isipokuwa” mama yao yupo hai na salama na anaishi Kenya! 'Mimi nilistuka na kushindwa jinsi ya kumjibu ila nilifurahi kwamba blog yangu imevumbua dhahabu iliyofichwa' na kwamba nitafanya juhudi kwa kushirikiana na wazalendo wenzangu tuwez

Kwa mwenendo huu, michezo haitafanikiwa Tanzania

Image
Mama Anna Kibira / Mwenyekiti wa Chama cha Netboli Taifa(CHANETA) Kuondolewa kwa timu ya taifa ya netiboli kwenye harakati za kutafuta tiketi ya kufuzu kushiriki fainali za Kombe la Dunia ni mwendelezo wa matukio ya kusikitisha yanayoendelea kuzikumba timu za taifa za Tanzania. Chama cha Netiboli Tanzania (Chaneta) kilitangaza kuiondoa timu hiyo kutokana na kukosa fedha za gabarone, Botswana kushiriki mashindano ya Afrika ya kutafuta tiketi ya kwenda Kombe la Dunia. Huenda kwa mara ya kwanza tungeshuhudia Taifa Queens ikikata tiketi ya kushiriki michuano hiyo mikubwa, lakini ndoto hizo ziliyeyushwa na Chaneta. Chaneta ilitembeza bakuli la kutafuta fedha za kufanikisha safari hiyo, lakini haikufanikiwa. Kushindwa kwa Taifa Queens kwenda kwenye mashindano hayo ni mwendelezo wa timu za Taifa kukosa mashindano muhimu. Shirikisho la Riadha Tanzania (RT) pia limekuwa likijiendesha kwa mtindo huo, hali kadhalika kwa vyama vya ngumi, kikapu, mpira wa meza, judo na

Malinzi maji ya shingo

Image
Jamal Malinzi / Rais wa Shirikisho la Mpira Tanzania (TFF) BODI ya Ligi Kuu Tanzania kwa kushirikiana na Klabu 14 za ligi hiyo, zimetishia kusaka theluthi mbili ya saini za Wajumbe wa Mkutano Mkuu wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), ili kuitisha Mkutano Mkuu wa dharura wa kupiga kura ya kutokuwa na imani Rais wa shirikisho hilo, Jamal Malinzi. Hayo yamesemwa jana jijini Dar es Salaam na wakili wa kujitegemea Dk. Damas Ndumbaro, anayeiwakilisha TPL Board na klabu 14 za Ligi Kuu, katika jaribio lao la kupinga shinikizo la TFF kuzikata klabu hizo asilimia tano ya pesa za wadhamini wa ligi hiyo ambao ni Kampuni ya Vodacom na Azam Media Ltd. Uamuzi huo wa TPL Board na klabu za Ligi Kuu, umekuja siku moja baada ya Malinzi kusisitiza kuwa uamuzi wa kukata asilimia tano ya makato ya pesa za wadhamni kwa klabu za ligi hiyo uko palepale, na kwamba bodi hiyo haina mamlaka ya kupinga agizo hilo na wenye uwezo au mamlaka hayo ni Kamati ya Utendaji ya TFF. Akijibu hoja moja baada ya nyi

HAKI: Michezo imezingatiwa katika rasimu inayopigiwa kura?

Image
Wajumbe wa bunge maalum la katiba linaloendelea Dodoma, bunge hilo linategemewa kufikia tamati muda hivi karibuni tena huenda lisifanikishe azma na matarajio ya watanzania. Hapana wanamichezo nafasi hatukupewa japo majina yalipendekezwa kuingizwa katika lile kundi la 201.  Hata hivo wanamichezo tusichukie wala kuhuzunika maana dalili zinaonyesha wazi kwamba hakuna maridhiano yatakayoleta katiba mpya kwa sasa. Mwisho wa siku sisi “Wanamichezo” tutakuwa na thawabu sababu hatukuthubutu kujadili jambo lisilowezekana maana dalili zipo wazi. Hata hivyo tuangalie kwa macho kwanza maana kuna msemo usemao “Anayesikiliza kwa makini ndiye anayefaidi mwishoni”.  Ombi kwa wawakilishi wetu bungeni hivi sasa ‘ Tafadhali waheshimiwa msiwe mabubu katika kupigania haki za wanamichezo kama ambavyo mnapigia kelele ufujaji wa fedha za uma' 'Mkumbuke kwamba jasho la mshezaji ni gharama zaidi kuliko noti zinazochapishwa na Federal Reserves’ Ninyi kushindwa kutuwakilisha vyema

Ikangaa apigiwa debe ‘kumrithi’ Malinzi uenyekiti wa BMT

Image
Col. Rt. Juma Ikangaa Mwanariadha wa zamani , Juma Ikangaa anatajwa kurithi nafasi ya uenyekiti  wa Baraza la Michezo la Taifa (BMT) baada ya Dioniz Malinzi kumaliza muda wake wa miaka mitatu juzi Jumapili.  Habari za ndani ambazo gazeti hili ilizipata zilieleza kuwa kati ya majina yaliyopendekezwa na Serikali, Ikangaa anapewa nafasi kubwa ya kuchukua mikoba ya Malinzi.  “Yalipendekezwa majina kadhaa ya watu maarufu ambao Serikali iliona wanastahili kuongoza BMT baada ya Malinzi kumaliza muda wake na Ikangaa ndiye anapewa nafasi kubwa ya kuwa mwenyekiti,” kilisema chanzo chetu.  Mwenyewe (Ikangaa) alipotafutwa na gazeti hili kujua msimamo wake, hakukubali wala kukataa kutaka cheo hicho zaidi ya kueleza hana taarifa zozote juu ya uteuzi huo. Gazeti hili lilimtafuta, Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Profesa Elisante Ole Gabriel ili k

Sugu atikisa Uwanja wa Sokoine

Image
Sugu sugu sugu… hivyo ndiyo mashabiki wa Mbeya City walivyoimba kwa muda mrefu baada ya mbunge wa Jimbo la Mbeya Mjini, Joseph Mbilinyi ‘Sugu’ kuingia uwanjani juzi kushuhudia mechi ya Ligi Kuu kati ya Mbeya City na Coastal Union. Ilikuwa katika dakika ya 38 ya mchezo huo, wakati Sugu alipoingia uwanjani na baada ya kushuka tu kwenye gari lake, uwanja mzima ulizizima kwa kelele za mashabiki kumshangilia kwa nguvu zote  wakisema “Sugu sugu sugu”, huku wakimtaka aende kukaa kwenye eneo walilokuwapo. Sugu alilikubali wito huo na kwenda kukaa eneo la mashabiki hao. Mmoja wa viongozi waliokuwa kwenye jukwaa kuu alishuka ghafla kwa lengo la kumkaribisha Sugu meza kuu, lakini Sugu hakwenda na badala yae alinyosha njia kwenda kukaa kwa mashabiki huku akishangiliwa kwa nguvu. Akizungumza na gazeti hili, baada ya kumalizika kwa mechi hiyo, Sugu alisema hakuwa na sababu yoyote ya kukaa jukwaa kuu kwani uhondo wa mchezo ni pale unapokuwa na vijana aliowaita wenye ‘mizuka’.

Uzembe waitoa Tanzania michezo ya Olimpiki 2016

Image
Tanzania haitashiriki michezo ya soka  kimataifa hadi mwaka 2016 kutokana na timu yake ya  vijana  wa umri chini ya miaka 23  kutoshiriki michuano ya kusaka  tiketi ya kushiriki Olimpiki  msimu wa 2015/2016. Kukosekana kwa timu hiyo ya U-23 kunaweza kuwa uzembe  wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF). Katika ratiba iliyotolewa juzi na Shirikisho la Soka  Afrika (CAF), pazia la michuano hiyo litafunguliwa Desemba. Katika michuano hiyo, raundi ya kwanza  Rwanda itaanza kukata utepe kwa kumenyana na Somalia wakati Kenya itacheza na Zambia au Botswana. Kikosi hicho mara ya mwisho kilishiriki michezo ya  Afrika mwaka 2011,  kikiwa chini ya Jamhuri Kihwelo ‘Julio’ na kiliondolewa mapema kwenye michuano hiyo na Nigeria.  Hata hivyo, U-23 haitashiriki michuano hiyo kwa vile Tanzania haikuthibitisha ushiriki wake huku viongozi wa juu wa TFF wakikwepa kulizungumzia  suala hilo.

Bodi ya ngumi iundwe kunusuru mabondia

Image
Rais wa TPBO Yassin Abdallah 'Ustadhi' akikabidhi vyeti Mchezo wa ngumi za kulipwa ni miongoni mwa michezo inayoongoza kwa kupendwa hapa nchini, tukiachilia mbali soka ambao unaongoza kupendwa zaidi. Licha ya mchezo wa ngumi za kulipwa kuwa na nafasi kubwa kwa mashabiki kinachosikitisha ni namna mabondia wa ngumi za kulipwa hapa nchini wanavyotumika kuwaneemesha wengine huku wao wakiambulia fedha ya madafu na wakati mwingine kudhulumiwa kabisa. Kumekuwa na matukio mengi ya mabondia kudhulumiwa ambayo nikianza kuyaorodhesha huenda ukurasa huu ukajaa na usitoshe, kwani imekuwa ni kawaida viongozi wa ngumi za kulipwa kuwatumia kama madaraja mabondia. Hiyo yote inachangiwa na mfumo wa uongozi wa ngumi za kulipwa tulionao hapa nchini, japo tunaambiwa ngumi za kulipwa ni biashara, lakini ubabaishaji umekithiri kwa viongozi wake kuendesha mchezo huo wanavyotaka wao. Huu utaratibu wa ngumi za kulipwa kusimamiwa na kampuni za TPBO Limited chini ya rais wake, Yassin Abdall

New force: A group of tennis coaches started academy

Image
Some of the 'Kijitonyama Tennis Academy' trainees pose for a group photo after the session It is clear that sports associations alone can’t improve sports development in any country unless other efforts are implemented on the sidelines. Tanzania Tennis Association TTA is in turmoil at the moment to the point that National Sports Council has summoned them to appear before the NSC. The set back did little to distract the focus of other committee members who also have coaching qualifications, the pocket of trainees have started Kijitonyama Tennis Academy to facilitate training needs to kids who are lacking such opportunities. TTA is currently led by Fina Mango and William Kallaghe after the resignation of Methusela Mbajo as a result of ongoing misunderstanding.  Kijitonyama Tennis Academy strategies are led by Musa Haruna, Ismail Said, Francis Simon, Rabii Hassan and Hassan Kassim. Hassan Kassim is also a member of Tanzania Tennis Association.

Sumaye: Tulikosea kufuta michezo shuleni

Image
Frederick Tluway Sumaye/Waziri Mkuu Mstaafu Waziri Mkuu Mstaafu wa Serikali ya Awamu ya Tatu, Frederick Sumaye amesema uongozi wao ulikosea kimsingi kufuta michezo shuleni. Mwishoni mwa 1996, Serikali kupitia aliyekuwa waziri mwenye dhamana ya michezo, Joseph Mungai ilipiga marufuku michezo yote kwenye shule za umma. Katika tangazo lake, Mungai ambaye alikuwa Mbunge wa Mufindi Kaskazini (CCM), alisema uamuzi huo ulichukuliwa ili kuepusha muda mwingi wa masomo uliokuwa ukipotea kwa wanafunzi kushiriki michezo. Mungai alieleza wakati ule kuwa wanafunzi nchini walihitaji muda wa saa 198 kwa ajili ya masomo kwa mwaka, lakini nyingi kati ya hizo zilipotea bure kwenye shughuli nyingine, zikiwamo michezo. Lakini, akizungumza na gazeti hili kwenye mahojiano maalumu nyumbani kwake, Kiluvya, wilayani Kisarawe, mkoani Pwani, Sumaye aliukosoa uamuzi huo. “Lazima nikiri kuwa ‘tuli-overreact’ (tulitoa uamuzi mkubwa mno) kufuta michezo katika shule zetu,” alisema Sumaye, ambaye anajianisha m

MICHEZO: Mpango wowote ule unahitaji utaalamu wake

Image
Wanariadha wa kimataifa wakifanya mazoezi nchini Marekani katika jimbo la Colorado Duniani kila kitu ni taaluma, lakini taaluma lazima iendane na Uadilifu, Utii, Uaminifu na Hekima. Kwa mfano mchezo wa riadha unahitaji utaalamu wa kujua ni wapi pa kufanyia mazoezi? Ndipo sasa mpango wa ujenzi wa miundo mbinu ya mazoezi yenyewe yaanze kufikiriwa. Mfano mzuri ni jinsi wanariadha wengi duniani wanapofunga safari kwenda sehemu zenye mwinuko au tuseme nyanda za juu (High Altitude) kama inavyoonekana katika picha hapo. Kwa utafiti wangu mwenyewe sehemu ambazo wanariadha wa kimataifa wanafurika kutafuta High Altitude ni Bonde la Uffa Kenya na jimbo la Colorado Marekani.  Tanzania ni sehemu nzuri sana ambapo laity viongozi wetu wa michezo wangeumiza vichwa kujenga kituo kikubwa cha michezo tungepata kundi kubwa la wageni wa ‘Athletic Tourism”  Hivyo basi; Sisi wadau wa michezo hapa Tanzania tunapambana kujenga kitu kama hiki hapo ichani (National Sports Village).

Trouble looms for TTA officials

Image
Fina Mango/TTA Vice President The National Sports Council (NSC) has given Tanzania Tennis Association (TTA) a seven-day ultimatum to provide details as to why the body has not reported to meetings which the council has been holding to solve wrangles in the association.   NSC officer Benson Chacha who is responsible for tennis desk confirmed that NSC has dispatched a letter to TTA leadership on the matter.   He said NSC has on four occasions invited TTA for meetings but neither showed up, nor gave any excuse.   ‘On Wednesday the Chairman of NSC was there waiting for them but they never showed up, so we have decided to write them to explain as to why they are failing to attend the meetings. NSC rules are clear on disciplinary action which can be taken on such cases, but we want the officials to explain and also defend themselves,’ he said.   According to Chacha, early this year some members of TTA complained to NSC on the way the association is run, the me

Zitto azitaka fainali za Afrika 2017

Image
Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe ameishauri Serikali isiache nafasi adimu ya kuandaa fainali za Mataifa ya Afrika 2017 (Afcon) baada ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kuliomba Shirikisho la Soka Afrika (Caf) kuwa mwenyeji. “Nimeona TFF wametangaza kuwa wanaomba kuandaa Afcon 2017, watu wameipokea kwa mtazamo tofauti. Hii ni nafasi ambayo hatutakiwi kuiacha, nchi yetu haijawahi kushiriki mashindano hayo tangu mwaka 1980,” alisema Zitto. Alisema: “Kuna njia mbili tu za kushiriki mashindano hayo, moja ni kufuzu na nyingine ni kuandaa fainali hizo.”  “Kwa upande wetu tangu mwaka 1980 tumejaribu, lakini tumeshindwa hivyo njia pekee ni kuandaa ili tushiriki. Hivi mnaijua nchi inayoitwa Burkina Faso? Wao waliandaa Afcon mwaka 1998, ni nchi maskini ya kutupwa. Tunachohitaji ni kujenga viwanja tu kwa sababu hoteli nzuri tunazo,” alisema Zitto.  Alisema kama yeye angekuwa, angeunda kamati maalumu ya kuomba zabuni hiyo ili kuhakikisha Tanzania inashinda kwa kuwa n