Posts

Showing posts with the label Riadha

Hatimaye RT wakabwa mahakamani kwa madai ya Milioni 20

Image
Suleiman Nyambui / Katibu mkuu wa Chama Cha Riadha Tanzania Kampuni ya SYMAITON SAPALI & CATHY CATERING imewaburuza viongozi wa Chama Cha Riadha Tanzania RT kwa deni la Tsh: 20,000,000 iliyotokana na chakula cha wanariadha wakati wa mashindano ya taifa yaliyofanyika Dar Es Salaam September 2012. Kesi hiyo (Civil Case Number 9/2014) ilifunguliwa katika mahakama ya wilaya ya Temeke siku za nyuma huku viongozi wa RT wakikaidi wito wa mahakama. Juzi (September 11, 2014) Katibu wa RT Suleiman Nyambui alihudhuria kesi hiyo baada ya mahakama kutoa amri kali ambapo angedharau amri hiyo huenda angekamatwa na kutiwa ndani. Akihojiwa na kituo kimoja cha redio hapo jana, Nyambui alikana kesi hiyo yenye kutia doa chama cha riadha, lakini muda mfupi baadae mwanasheria wa RT Thabit Bashir alithibitisha kuwepo kwa kesi hiyo. Hivi karibuni Suleiman Nyambui amekuwa akiandamwa kote kote hadi kutiliwa shaka katika biashara ya madawa ya kulevya!  Akisthibitisha yeye mw

Nyambui ataka kung’atuka RT

Image
Katibu wa Chama cha Riadha Tanzania (RT), Suleiman Nyambui amemtaka mtu yeyote anayeweza kuongoza chama hicho ajitokeze ili yeye ang’atuke na kumwachia madaraka. Nyambui alisema katika mahojiano kuwa yuko tayari kujiuzulu wadhifa huo ndani ya RT kama atatokea mtu ambaye anadhani akimwachia cheo hicho ataweza kuleta mafanikio katika mchezo huo. Kigogo huyo wa RT alisema amekuwa akifanyiwa fitina na baadhi ya watu waliowahi kumshawishi kuungana nao ili wapate fursa ya kuitumia RT kufanya maovu yao, lakini walipokumbana na ‘kigingi’ chake wameanza kumfanyia fitina. “Baadhi ya watu wananizungumzia vibaya. Lakini niko tayari kuondoka RT hata leo kama mimi ndiyo kikwazo cha mafanikio ya riadha endapo tu akitokea mtu ambaye atanithibitishia kuwa ana uwezo wa kuleta mafanikio,” alisema Nyambui. CHANZO: Mwananchi

Filbert Bayi aishangaa Serikali

Image
Katibu Mkuu wa Kamati ya Olimpiki Tanzania (TOC), Filbert Bayi amesema ripoti ya timu za Tanzania zilizoshiriki michezo ya Jumuiya ya Madola imekwama baada ya Serikali kutaka wanamichezo wote waliokwenda Scotland kuhusishwa wakati itakapowasilishwa kwao. Bayi alisema Serikali imetaka wachezaji walioshiriki kwenye michezo hiyo kuwepo wakati vyama vyao vikiwasilisha ripoti zao za Madola. “Ripoti zimechelewa kwa kuwa Serikali imetaka wanamichezo wote waliokuwa Scotland kuwapo katika kikao cha tathmini, hiyo ni gharama, hivyo tuko kwenye mchakato wa kutafuta fedha ili kufanikisha hilo,” alisema. Alisema gharama za kufanya tathmini hiyo ni Sh 8 milioni, ambazo pia zitatumika kuwagharamia wachezaji wa mikoani walioshiriki michezo hiyo kuja Dar es Salaam ili kushiriki katika tathmini hiyo. “Hii ni mara ya kwanza ripoti ya Madola na tathmini yake kufanyika kwa kushirikis

Lipumba: Tuwekeze katika michezo

Image
Ni ndoto kwa Tanzania kufanya vizuri kwenye michezo kitaifa na kimataifa bila kuwekeza kwenye kukuza vipaji vya vijana kama ambavyo zimefanya nchi nyingine duniani. Huo ni ushauri wa Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi (CUF), Profesa Ibrahim Lipumba katika mahojiano maalumu na gazeti hili mwishoni mwa wiki. Prof Lipumba, ambaye mbali ya kubobea katika uchumi na siasa, alisema Tanzania haina budi kuwekeza katika michezo kuanzia elimu ya awali, msingi, sekondari hadi vyuo vikuu ambako vipaji vipya vitaweza kuibuliwa. Alisema Tanzania imekuwa ikifanya vibaya kimichezo kutokana na watoto wake wengi kudumaa kimwili kutokana na lishe duni kwao na wazazi wao. “Tunafanya vibaya kimichezo, tunatafuta sababu, lakini sababu zipo katikati yetu,” alieleza Prof Lipumba na kuongeza kuwa asilimia 42 ya watoto nchini wamedumaa, jambo ambalo linawaathiri katika mambo mengi yakiwamo michezo. Msomi huyo ambaye ni shabiki wa klabu ya Simba alisema uwekezaji ambao umefanywa kwa mfano n

Viongozi wa riadha Tanzania wakubali makosa

Image
Tulitegemea Shirikisho la Riadha la Taifa (RT) lingeyatumia mashindano hayo kuanza kutengeneza timu ya ushindani ambayo itashiriki kwenye Michezo ya Afrika mwakani.PICHA|MAKTABA  Shirikisho la Riadha Tanzania (RT) limeshindwa kupeleka wanamichezo kwenye mashindano ya Afrika ya riadha yaliyomalizika wiki iliyopita jijini Marrakech, Morocco na kushirikisha wanariadha 600 kutoka mataifa 47. Mashindano hayo yalifanyika kwa siku nne, kuanzia Agosti 10 mpaka 14 huku Afrika Kusini ikiongoza kwa kutwaa medali nyingi, ikifuatiwa na Nigeria na Kenya. Katika mashindano hayo, Zanzibar ilipeleka wanariadha wawili waliochuana katika michezo ya kurusha kisahani, mkuki na tufe huku Bara ikishindwa kupeleka mkimbiaji hata mmoja. Kitendo cha Bara kushindwa kupeleka wanamichezo katika mashindano hayo ya riadha ya Afrika kimewanyima fursa wanariadha kwenda kushindana na kutafuta viwango vitakavyowasaidia kwenye mashindano mengine ya kimataifa. Mashindano hiyo ya riadha

Ikangaa, Shahanga waishangaa RT

Image
Kanali Mstaafu Juma Ikangaa Bingwa wa Afrika wa 1982, Juma Ikangaa na mshindi wa medali fedha ya Jumuiya ya madola, Gidamis Shahanga wamelishangaa Shirikisho la Riadha Tanzania (RT) kushindwa kupeleka timu kwenye Mashindano ya Afrika yanayoendelea nchini Morocco. Wanariadha hao wakongwe wamesema kuwa, kati ya vioja vinavyofanywa na RT ni kushindwa kupeleka timu kwenye mashindano makubwa kama hayo na kusisitiza kuwa kutokwenda kwenye mashindano hayo kutaiweka Tanzania katika mazingira magumu  kwenye Michezo ya Afrika (All African Games) mwakani. Gidamis Shahanga Wakizungumza na gazeti hili kwa nyakati tofauti jana, walisema, Tanzania ilipaswa kutumia mashindano ya Afrika kuwapima wanariadha wake kwa maandalizi ya Michezo ya Afrika. “RT imekosea kutopeleka timu Morocco, tunaambiwa imepeleka wanariadha wawili ambao  wamekwenda kuiwakilisha Zanzibar na si Tanzania bara,” alisema Ikangaa aliyewahi kuwa bingwa wa marathoni kwenye mashindano hayo ya 1982, nchini Mi

Tunasubiri aibu tena: Medali ngumu Olimpiki ya Vijana

Image
Kwa mazingira haya ya mazoezi Tanzania itasubiri sana ushindi wa kupata medali. Makocha wa timu za Tanzania kwenye Olimpiki ya Vijana, wamesema wana kibarua kigumu cha kuhakikisha wanarejea na medali kwenye michezo hiyo itakayoanza Jumamaosi nchini China. Msafara wa wachezaji wanne na viongozi watatu uliondoka jana jioni na ndege ya Shirika la Qatar, na utakwenda moja kwa moja jijini Nanjing inapofanyika michezo hiyo. Wakizungumza na gazeti hili kwa nyakati tofauti, kocha wa timu ya riadha, Mwinga Mwanjala na mwenzake wa timu ya kuogelea, Ally Hamis Bamba walisema wana kibarua kigumu kwenye mashindano hayo. “Tunakwenda kushindana, lengo letu ni kuhakikisha tunashinda, kila nchi inahitaji medali na wachezaji wetu pia wanahitaji medali, tuna kibarua kigumu cha kuhakikisha tunapambana ili kushinda,” alisema Bamba. Wakati kocha wa riadha, Mwinga Mwanjala akisema wanakwenda kwenye mashindano hayo kama washindani, hivyo wanaamini nafasi ya kushinda wanayo.“Bahati nzuri mi

KAULI YA NYAMBUI NI KIPIMO TOSHA CHA UDHAIFU WA UZALENDO WETU

Image
Suleiman Nyambui / Mtanzania asiyejali sheria wala uzalendo KATI ya vipindi vya michezo redioni ambavyo hunipita kwa nadra sana ni kile cha Radio One Stereo. Siku chache zilizopita, nilikuwa nikifuatilia namna Maulid Kitenge alivyokuwa akimhoji Katibu Mkuu wa Chama cha Riadha Tanzania (RT), Selemani Mujaya Nyambui. Kitenge alikuwa akitaka kujua sababu ya timu ya Tanzania iliyoshiriki michuano ya Jumuiya ya Madola kurejea nyumbani bila ya hata kipande cha medali. Nyambui ambaye katika sauti yake unaweza kubaini mengi, alizungumza mambo ya ajabu ambayo hauwezi kutarajia kiongozi au mwanamichezo mwenye sifa yake anaweza kuzungumzia. Mwanariadha huyo wa zamani ambaye unaweza kumwita ni kati ya mashujaa waliowahi kuchukua medali na kuileta nyumbani kupitia michuano ya Olimpiki, alikuwa akizungumza sawa na mtu aliyekuwa hayuko vizuri, labda kwa uchovu au ni yule asiyejali tu. Wakati Kitenge akieleza alitaka kujua kwa nini timu hiyo haikuleta medali, Nyambui hakufafanua lo

Glasgow: Emiliani anyukwa, Ikangaa, Bazil leo

Image
Dar es Salaam. Bondia Emiliani Patrick ameendeleza rekodi mbaya ya Tanzania kwenye michezo ya Jumuiya ya Madola baada ya jana kupokea kipigo kutoka kwa Mganda Bashir Nasir. Bondia Emiliani Patrick aliaga kwenye michezo hiyo baada ya kuruhusu kipigo cha pointi za majaji 2-1 dhidi ya Mganda huyo. Katika pambano hilo, Emiliani alipata matokeo ya pointi 28-29 raundi ya kwanza, 27-30 na raundi ya mwisho aliongoza kwa pointi 29-28. Kwa matokeo hayo sasa mategemeo ya Tanzania walau kutwaa medali kwenye michezo hiyo yamesalia kwa wanamichezo watatu. Hadi jana, wanamichezo 36 wa Tanzania walioshiriki ngumi, riadha, judo, mpira wa meza, kunyanyua vitu vizito, kuogelea na baiskeli walikuwa tayari wameondoshwa kwenye mashindano hayo. Tegemeo pekee kwa Tanzania lipo kwa wanariadha, Dotto Ikangaa na Bazil John watakaochuana katika mbio za kati za mita 1,500 na bondia, Hamad Furahisha aliyetarajiwa kuzichapa jana usiku. Kwa mujibu wa meneja wa timu za Tanzania kwenye mic

Glasgow: BMT na RT wametupotezea medali zetu watanzania, wamlaghai JK

Image
Siku ya kuagwa timu ya Tanzania ya Jumuiya ya Madola rais Jakaya Kikwete hakutaarifiwa kwamba viongozi wa RT walichaguliwa kinyume cha katiba na pia kinyume cha sheria # 12 iliyotungwa na bunge 1967. Lakini pia waziri Bernard Membe amejikuta akitoa pesa za watanzania kwa wahuni waliodharau katiba ambayo ndiyo msingi wa kila kitu. Ningepata wasaa wa kumuuliza waziri Membe ningemuuliza kwamba 'Ni kwa nini hakusumbuka kupeleleza uhalali wa RT'? Hata hivyo nampa pongezi hili 'Thanks BUT no thanks Hon. Membe' kwa kuwa ametoa pesa ambazo zilitumika kubagua wanamichezo sababu wanariadha waliokwenda kambi za nje HAWAKUSHINDANISHWA na wenzao ili kubaini nani bora atakayeweza kuiletea Tanzania medali. Kwa maana nyingine waziri ameshiriki kubariki RT kubagua uwepo wa wanawake katika timu ya riadha ya taifa 'Ama kwa kujua ama bila kujua' Kenya kwa siku ya jana tu wamekusanya medali TANO, Uganda nao wamenyakua medali lakini sisi tunamdanganya rais wetu!   &

Tunasubiri ‘Matokeo Makubwa Sasa’

Image
Safari hii, serikali kwa kutumia uhusiano wake wa kitamaduni na nchi za China, Uturuki, Ethiopia na New Zealand iliweza kutuma wanamichezo wake kwenye nchi hizo tofauti kulingana na mazingira mazuri ya mchezo fulani ili waweze kujiandaa ipasavyo. Tanzania ni miongoni mwa nchi ambazo bendera yake itapepea jijini Glasgow, Scotland katika ufunguzi wa Michezo ya Jumuiya ya Madola itakayofanyika Julai 23 kwenye Uwanja wa Celtic Perth. Michezo hiyo muhimu hushirikisha nchi wanachama wa jumuiya hiyo ambazo ziliwahi kuwa koloni la Uingereza na mwaka huu inatarajiwa kushirikisha mataifa 71 ambayo yatachuana katika michezo 17 tofauti itakayofikia tamati Agosti 3. Katika michezo hii Tanzania inatarajiwa kuwakilishwa na wanamasumbwi, wanariadha, kunyanyua vitu vizito, mpira wa meza, wachezaji judo, waendesha baiskeli na waogeleaji ambao tayari wameshawasili kwenye kijiji cha michezo nchini Scotland tayari kwa mi

Nyambui: Niliomba nifungwe miaka 100 jela

Image
Kocha wa timu ya taifa ya riadha na Katibu Mkuu wa Shirikisho la Riadha Tanzania (RT), Suleiman Nyambui amesema aliomba afungwe miakba 100 jela kama ikibainika anajihusisha na usafirishaji wa dawa za kulevya. Kocha huyo mpya wa timu ya taifa alisema bado anateswa na ‘mzimu’ wa kashfa ya kusafirisha dawa za kulevya iliyowahi kumkabili, kashfa iliyoichanganya familia yake na yeye mwenyewe. Nyambui aliliambia gazeti hili katika mahojiano maalumu kuwa, katika maisha yake ya riadha tangu akikimbia miaka 1970 hadi hivi sasa akiwa ni kocha na katibu mkuu, hakuna changamoto kubwa ambayo hataisahau kama siku alipoitwa kuhojiwa juu ya tuhuma hiyo. Kigogo huyo wa RT alisema alijikuta akiingia matatani na kuhojiwa na kitengo cha kudhibiti dawa za kulevya hapa nchini kwa saa sita mfululizo juu ya kuhusika kwake na uuzaji na usafirishaji wa dawa za kulevya. “Kiukweli watu wa kitengo cha kudhibiti  dawa  za kulevya walikuwa na vielelezo vyote vya nam

Umuhimu wa Katiba: Riadha taifa ni aibu

Image
Ukistaajabu ya Mussa, utayaona ya Firauni! Ndivyo ilivyokuwa kwenye mashindano ya taifa ya riadha yaliyoanza jana kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam. Licha ya kukosa msisimko, aibu nyingine imelikumba Shirikisho la Riadha Tanzania (RT), baada ya kukosekana kwa vijiti vya relay, namba za kukimbilia na vibendera vinavyotumika kwenye mashindano wakati wa mbio za ufunguzi hapo jana. Gazeti hili lililokuwepo uwanjani hapo tangu mbio zinaanza lilishuhudia mmoja wa wadau wa RT akijitolea kofia yake yenye rangi nyekundu iliyotumika  kama kibendera sambamba na waandaaji kutumia karatasi nyeupe kama kibendera kingine. Wakati wa mbio za mchujo za mita 100 mara nne, wakimbiaji walilazimika kutumia mbao zenye mfano wa vijiti vya relay kutokana na kutokuwepo kwa vijiti  halisi vya mbio hizo. Kocha Shaban Hiki alipoulizwa juu ya vijiti hivyo alisema ni vya muda na vimetengenezwa ili viokoe jahazi. “Vijiti halisi tumeambiwa vimeibwa hivyo vimetengenezwa hivi ‘local’,” a

Riadha Taifa madudu, nyota wa Madola hoi

Image
MASHINDANO ya taifa ya riadha yalianza jana katika Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam huku yakigubikwa na dosari nyingi, ikiwemo wanariadha watakaoshiriki mashindano ya Jumuiya ya Madola kuchemka. Kushindwa huko kumekuja ikiwa ni siku chache kabla ya timu ya Tanzania kuondoka nchini kwenda mjini Glasgow, Scotland kwa mashindanbo hayo yatakayoanza Julai 23 hadi Agosti 3. Miongoni mwa dosari katika mbio za mwaka huu, ni maandalizi duni yaliyofanywa na Riadha Tanzania (RT) kwani baadhi ya wanariadha wameendelea kukimbia bila viatu kama mwaka jana. Baadhi ya wanariadha jana walishiriki mbio hizo bila jezi rasmi, wengine wakivalia jezi za soka kwa mfano Kiabo Kahorwe kutoka Shinyanga. Kahorwe alisema amefanya hivyo kwa kukosa fedha za kununua vifaa, hivyo kwa vile anaupenda mchezo huo, akaamua kujitafutia nauli tu ya kumpeleka Dar es Salaam na kurejea kwao. Wengine walionekana wakishiriki wakiwa wametinga gauni, sketi na blauzi, huku baadhi yao wakiwa peku na wengine w

MSIBA MKUBWA: Mwili wa Saria kuagwa leo

Image
MWILI wa aliyekuwa mwanariadha, kocha na kiongozi wa zamani wa Riadha Tanzania (RT), Ernest Saria aliyefariki usiku wa kuamkia Jumanne, unatarajiwa kuagwa leo saa 3 asubuhi katika kituo cha Polisi, Kurasini jijini Dar es Salaam. Akithibitisha hilo jijini Dar es Salaam jana, Katibu Mkuu wa RT, Suleima Nyambui alisema, shughuli za kuagwa kwa mwili wa marehemu, zitaanza saa tatu asubuhi katika kituo hicho kabla ya kusafirishwa kupelekwa mjini Moshi, Mkoani Kilimanjaro. Saria alifikwa na umauti huo akiwa nyumbani kwake, Pugu jijini Dar es Salaam, bada ya kuugua maradhi ya malaria na dengue. Katika uhai wake, Saria aliwahi kushika nyadhifa mbalimbali katika mchezo wa RT ikiwemo ya Katibu wa Kamati ya Ufundi ya RT na Mjumbe wa Kamati ya Utendaji hadi mwaka juzi, alipowania nafasi ya Makamu wa Pili wa Mwenyekiti Ufundi. Aidha, wakati wa ujana wake aliwahi kuwa bingwa wa mbio za meta 400 na 800 nchini na kuipeperusha nchi katika mashindano mbalimbali ya kimataifa na

Angela Kairuki: Atakayevunja rekodi riadha taifa mil. 1/-

Image
NAIBU Waziri wa Sheria na Katiba, Angela Kairuki, ameahidi zawadi ya shilingi milioni moja kwa atakayevunja rekodi katika mashindano ya riadha ya taifa yatakayofanyika Juni 12 na 13, jijiji Dar es Salaam. Ahadi hiyo ilitolewa jana na naibu waziri huyo wakati akifunga semina ya waamuzi 22 watakaoendesha mashindano hayo na kuongeza kuwa wanariadha wanahitaji sapoti waweze kufanya vizuri kitaifa na kimataifa. “Michezo inakuza uchumi, pia ni sehemu ya maisha ya binadamu, ni muhimu tukiwa tunawapa sapoti wanariadha mbalimbali, hivyo mimi kama mdau wa mchezo huo naahidi kutoa hela hiyo ili aendelee kuwa mwanariadha bora,” alisema. Alisema serikali itaendelea kuwasaidia wanamichezo katika mipango yao ili kurudisha heshima ya nchi kwa wanariadha wake kufanya vizuri kama ilivyokuwa kwa Filbert Bayi, Suleimani Nyambui na wengineo. Mwenyekiti wa Chama cha Riadha Mkoa wa Dar es Salaam (DAA), Zainabu Mbiro, alisema waamuzi walioshiriki seminda hiyo ni kutoka mikoa mbalimbali ikiwa

SHABANI HIKI: Ninaimani timu ya riadha itailetea heshima Tanzania

Image
Timu ya wanariadha waliokuwa Ethiopia kwa mazoezi ya maandalizi ya mashindano ya Jumuia za Madola imerejea nchini jana. Katikati ni kocha aliyefuatana na timu Ndg. Shabani Hiki. Wanariadha hao waliowasili nchini kupitia uwanja wa ndege wa Mwalimu Julius Nyerere waliahidi kuiletea heshima Tanzania kwa kuzoa medali katika mashindano yatakayofanyika Glasgow Scotland mwishoni mwa mwezi huu wa July. Mwanzoni mwa mwezi June mwaka huu serikali ilitoa fedha za makambi kupitia wizara ya Mambo ya Nje katika harakati za kuinusuru Tanzania kupata medali katika mashindano hayo ya Commonwealth Games yajulikanayo pia kama "Family Games" zinazoshirikisha nchi zote zilizowahi kuwa chini ya himaya ya Uingereza.